Tanzania Bara vs Burkina Faso Leo 09/01/2025 Saa Ngapi?
Timu ya Soka ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars) inatarajia kuwakabili Burkina Faso katika mechi ya kukamilisha ratiba ya mashindano ya Kombe la Mapinduzi itakayochezwa leo, Januari 9, 2025, kwenye Uwanja wa Gombani, kisiwani Pemba.
Mechi hii ni sehemu ya hatua za awali za mashindano hayo, huku Kilimanjaro Stars ikipambana kutafuta ushindi wa heshima utakao ondoa haibu ya kumaliza michuano hii bila ushindi baada ya matokeo yasiyoridhisha kwenye michezo yao miwili ya awali.
Kilimanjaro Stars, chini ya uongozi wa Kocha Mkuu Hamad Ally, imekuwa na safari ngumu katika mashindano haya. Timu hiyo ilianza kwa kufungwa bao 1-0 na wenyeji Zanzibar Heroes kwenye mchezo wa ufunguzi, na kufuatia kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa Kenya katika mechi ya pili. Matokeo haya yameifanya Tanzania Bara kupoteza nafasi ya kuendelea hadi hatua za mtoano. Hivyo, mchezo wa leo ni wa kukamilisha ratiba pekee kwa Kilimanjaro Stars.
Kwa upande wa Burkina Faso, mechi ya leo ni ya muhimu zaidi. Timu hiyo ina pointi nne, sawa na Kenya, na wanahitaji ushindi au sare ili kujihakikishia nafasi ya kucheza fainali ya mashindano haya, ambayo itafanyika Januari 13, 2025. Hali hii inafanya mchezo wa leo kuwa na ushindani mkubwa kwao, wakitafuta nafasi ya kutwaa ubingwa wa Kombe la Mapinduzi.
Mchezo wa Leo Saa Ngapi?
Mchezo kati ya Tanzania Bara na Burkina Faso unatarajiwa kuanza saa 1:00 usiku katika Uwanja wa Gombani. Huu ni muda mzuri kwa mashabiki wa soka kufika uwanjani kushuhudia burudani ya soka na kuona iwapo Kilimanjaro Stars itaweza kupata ushindi wa kwanza au kufunga bao lao la kwanza kwenye mashindano haya.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Kilimanjaro Stars Kukamilisha Ratiba Mapinduzi Cup Dhidi ya Burkina Faso
- Shassir Nahimana (31) Atambulishwa Rasmi na Pamba Jiji
- Msimamo Wa Kundi Mapinduzi Cup 2025
- Msimamo wa Kundi la Yanga Klabu Bingwa Afrika CAF 2024/2025
- Ratiba ya Kombe la Mapinduzi 2025
- Shaban Chilunda Awindwa na KMC
- Vita ya Kumsajili Okoyo Yazuka Kati ya KMC, Mashujaa na Namungo
- Guede Afunguka Sababu za Kutemwa Singida Black Stars
Leave a Reply