Tangazo la Kuitwa Kwenye Usaili MDAs NA LGAs 2025 | MDAs & LGAs Call For Interview March 2025
Ofisi ya Rais wa Jamhuri, Sekretarieti ya Ajira na Uchaguzi wa Utumishi wa Umma ilitoa taarifa rasmi na kuwafahamisha wagombea waliochaguliwa kushiriki usaili wa nafasi mbalimbali katika taasisi za umma. Tangazo hili linafafanua tarehe, wakati na mahali pa mahojiano, pamoja na maagizo muhimu kwa washiriki.
Tangazo la Kuitwa Kwenye Usaili MDAs NA LGAs 2025
Tarehe na maeneo ya interview
Usaili utafanyika kuanzia March 17, 2025 hadi March 29, 2025 katika vituo mbalimbali vilivyotajwa katika wito wa maombi. Kila mshiriki lazima athibitishe jina lake, nafasi aliyoomba na mahali pa usaili kupitia orodha iliyotolewa/Tangazo la Kuitwa Kwenye Usaili MDAs NA LGAs 2025.
Maelekezo ya Kuzingatia kwa Wasailiwa
-
Usaili utafanyika kuanzia tarehe kama ilivyoainishwa kwenye tangazo hili, katika muda na sehemu zilizobainishwa kwa kila kada.
-
Kila msailiwa anatakiwa kufika kwenye eneo la usaili akiwa amevaa barakoa (mask).
-
Kila msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho halisi kwa ajili ya utambuzi.
-
Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:
- Kitambulisho cha Mkazi
- Kitambulisho cha Mpiga Kura
- Kitambulisho cha Kazi
- Kitambulisho cha Uraia
- Hati ya Kusafiria
- Leseni ya Udereva
- Barua ya utambulisho kutoka Serikali ya Mtaa/Kijiji unachotoka.
-
Wasailiwa wanatakiwa kufika na vyeti vyao halisi, kuanzia:
- Cheti cha kuzaliwa
- Cheti cha Kidato cha IV
- Cheti cha Kidato cha VI
- Vyeti vya Astashahada, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea kulingana na sifa za mwombaji.
-
Wasailiwa watakaowasilisha Testimonials, Provisional Results, Statement of Results, au Hatiza Matokeo za Kidato cha IV na VI (Form V and Form VI Results Slips) hawataruhusiwa kuendelea na usaili.
-
Kila msailiwa atajigharamia chakula, usafiri na malazi.
-
Kila msailiwa azingatie tarehe, muda, na mahali alipopangiwa kufanya usaili.
-
Waombaji waliomaliza masomo nje ya Tanzania wanapaswa kuhakikisha vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na mamlaka husika kama TCU, NACTE, na NECTA.
-
Waombaji kazi ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakukidhi vigezo, hivyo hawapaswi kusitisha kutuma maombi katika nafasi zijazo.
-
Kwa kada ambazo zinahitaji usajili wa kitaaluma, wasailiwa wanapaswa kuja na vyeti halisi vya usajili pamoja na leseni za kufanyia kazi.
-
Wasailiwa wote walioitwa kwenye usaili wanatakiwa kuhakikisha wanaingia kwenye akaunti zao na kunakili namba za mtihani, kwani namba hizo hazitatolewa siku ya usaili/Tangazo la Kuitwa Kwenye Usaili MDAs NA LGAs 2025.
Mapendendekezo ya Mhariri
Leave a Reply