TANESCO: Ratiba ya Kukatika Umeme Julai 3-4, Mikoa Itakayo Kosa Umeme Tarehe 3 na Tarehe 4 Julai 2024
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limetangaza taarifa ya kukosekana kwa huduma ya umeme kwa mikoa 15 nchini tarehe 3 na 4 Julai 2024. Kukatika huku kumepangwa kufanyika kuanzia saa 1:00 asubuhi hadi saa 12:00 jioni katika mikoa husika.
TANESCO: Ratiba ya Kukatika Umeme Julai 3-4, Mikoa Hii Kuathirika
Sababu ya Kukatika Umeme
TANESCO imesema kuwa kukatika huku kunasababishwa na kuzimwa kwa njia kuu ya kusafirisha umeme ya msongo wa kilovoti 220 kutoka Msamvu hadi Dodoma (SGR). Kuzimwa huku ni ili kuruhusu mkandarasi wa TRC (Tanzania Railways Corporation) kumalizia kazi zilizobaki kwenye vituo vya treni vya msongo wa kilovoti 220/33.
Mikoa Itakayo Kosa Umeme Tarehe 3 na Tarehe 4 Julai 2024
Mikoa itakayoathirika na kukatika kwa umeme ni:
- Iringa
- Njombe
- Ruvuma
- Mbeya
- Songwe
- Singida
- Shinyanga
- Simiyu
- Tabora
- Mwanza
- Mara
- Geita
- Arusha
- Kilimanjaro
- Manyara
Athari kwa Wananchi na Biashara
Kukatika kwa umeme kunatarajiwa kuathiri shughuli za kila siku za wananchi na biashara katika mikoa husika. TANESCO inawaomba wananchi kuwa wavumilivu wakati huu ambapo inafanya kazi ya kuhakikisha umeme unarejea haraka iwezekanavyo.
Faida za Kazi ya Matengenezo
TANESCO imesema kuwa kazi hii ya matengenezo ni muhimu ili kuimarisha mifumo ya uendeshaji treni na pia kuimarisha ufatiliaji na uendeshaji wa njia ya umeme ya 220kv Msamvu – Dodoma SGR.
Maelezo ya Ziada
TANESCO itaendelea kutoa taarifa kuhusu maendeleo ya kazi ya matengenezo na kurejeshwa kwa huduma ya umeme. Wateja wanaweza kuwasiliana na huduma kwa wateja wa TANESCO kwa maswali au maelezo zaidi.
Mapendekezo ya Mhariri:
Leave a Reply