Takwimu za Yanga Katika Ligi ya Mabingwa Afrika 2024/2025

Takwimu za Yanga Katika Ligi ya Mabingwa Afrika

Takwimu za Yanga Katika Ligi ya Mabingwa Afrika 2024/2025

Safari ya Yanga katika Ligi ya Mabingwa Afrika msimu wa 2024/2025 imekumbwa na changamoto nyingi, ikikosa nafasi ya kusonga mbele baada ya kutoka sare tasa dhidi ya MC Alger. Licha ya juhudi na umahiri wao, walimaliza hatua ya makundi wakiwa na pointi nane, ambazo hazikutosha kutinga robo fainali. Huu hapa ni muhtasari wa takwimu muhimu zinazodhihirisha safari yao kwenye mashindano haya yenye hadhi kubwa barani Afrika.

Katika hatua ya makundi, Yanga iliweza kushinda mchezo mmoja pekee nyumbani. Ushindi huo ulikuwa dhidi ya TP Mazembe ya DR Congo kwa mabao 3-1 tarehe 4 Januari 2025. Hata hivyo, walipoteza mchezo mmoja na kutoka sare mmoja, wakikusanya jumla ya pointi nne tu kati ya tisa walizoweza kuvuna kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Takwimu za Yanga Katika Ligi ya Mabingwa Afrika 2024/2025

Pointi na Mafanikio

Yanga imekusanya pointi nane msimu huu, idadi sawa na ile waliyopata msimu uliopita walipofuzu robo fainali. Hata hivyo, safari hii pointi hizo hazikutosha, kwani walimaliza nafasi ya tatu nyuma ya Al Hilal ya Sudan (pointi 10) na MC Alger ya Algeria (pointi 9).

Tangu kuanza kushiriki mashindano ya ngazi ya klabu barani Afrika, Yanga imefikia hatua ya makundi mara sita: mara tatu katika Ligi ya Mabingwa Afrika na mara mbili katika Kombe la Shirikisho Afrika. Katika hizo, mara mbili walifanikiwa kusonga mbele hadi robo fainali, huku mara nne wakikwama kwenye hatua ya makundi.

Wafungaji Bora wa Yanga

Mabao ya Yanga katika hatua ya makundi yalifungwa na wachezaji Clement Mzize na Stephane Aziz Ki, kila mmoja akifunga mabao mawili katika ushindi wa 3-1 dhidi ya TP Mazembe. Bao lingine lilifungwa na Prince Dube. Hii inawafanya Mzize na Ki kuwa wafungaji bora wa timu katika kampeni ya msimu huu.

Stephane Aziz Ki ameibuka kuwa mchezaji muhimu kwa Yanga katika mashindano haya. Akiwa na wastani wa mashuti 2.3 yaliyolenga lango kwa kila mechi, Ki ameongoza kikosi kwa idadi ya mashuti yaliyolenga lango, huku asilimia 44 ya mashuti yake yakilenga moja kwa moja.

Yanga imekuwa na wastani wa kupiga pasi 362 kwa kila mechi, ikiwa na usahihi wa asilimia 80.2. Takwimu hizi zinawaweka nafasi ya nne nyuma ya vigogo wa Afrika kama Mamelodi Sundowns, Al Ahly, na Pyramids FC. Katika upande wa krosi, Yanga imepiga wastani wa krosi nne kwa mechi, sawa na asilimia 22.4 za usahihi, ikiweka nafasi ya sita miongoni mwa timu za mashindano haya.

Changamoto Katika Utekelezaji

Timu imepoteza nafasi tisa za wazi katika mechi sita za hatua ya makundi dhidi ya MC Alger, Al Hilal, na TP Mazembe. Zaidi ya hayo, Yanga imefanikiwa kupata kona 48 katika mechi hizo, ikiwa na wastani wa kona nane kwa kila mechi.

Umuhimu wa Djigui Diarra

Kipa wa Yanga, Djigui Diarra, amekuwa nguzo muhimu katika safu ya ulinzi. Akiwa nafasi ya 13 kwenye chati ya makipa waliokoa hatari nyingi, Diarra ameokoa asilimia 60 ya mashambulizi yaliyolenga lango lake.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Kariakoo Dabi Kupigwa Kwa Mkapa Machi 8
  2. Msimamo Kundi la Simba Kombe la Shirikisho CAF 2024/2025
  3. Matokeo ya Simba SC vs CS Constantine Leo 19/01/2025
  4. Kikosi cha Simba SC vs CS Constantine Leo 19/01/2025
  5. Yanga vs MC Alger Leo 18/01/2024 Saa Ngapi?
  6. Matokeo ya Yanga vs MC Alger Leo 18/01/2024
  7. Kikosi cha Yanga vs MC Alger Leo 18/01/2024
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo