Tabora United VS Yanga Leo 02/04/2025 Saa Ngapi?

Tabora United VS Yanga Leo 02 04 2025 Saa Ngapi

Tabora United VS Yanga Leo 02/04/2025 Saa Ngapi?

Leo tarehe 2 Aprili 2025, Tabora United itapambana na mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya NBC, Yanga SC, katika Uwanja wa Ally Hassan Mwinyi, Tabora. Mchezo huu ni sehemu ya raundi ya 23 ya ligi na unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Katika mchezo wa awali wa msimu huu, Tabora United ilishangaza Yanga kwa kushinda 3-1. Hata hivyo, Yanga sasa ipo chini ya kocha mpya, Miloud Hamid, na imekuwa ikionyesha ubora mkubwa kwa kushinda mechi nne kati ya tano za mwisho za ligi. Kwa upande wa Tabora United, sasa inanolewa na kocha Genesis Mang’ombe kutoka Zimbabwe, ikipambana kuhakikisha inabaki katika nafasi za juu.

Yanga inahitaji ushindi ili kuimarisha nafasi yake kileleni kwa kufikisha pointi 61, huku Tabora United ikisaka pointi tatu ili kufikisha pointi 40 na kujiweka karibu na nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi.

Taarifa za Mchezo

  • Timu: Tabora United vs Yanga SC
  • Tarehe: 02/04/2025
  • Saa: 4:15 PM
  • Uwanja: Ally Hassan Mwinyi, Tabora

Tabora United VS Yanga Leo 02/04/2025 Saa Ngapi?

Mashabiki wa soka wanatarajia kuona mchezo wenye ushindani mkubwa, huku kila timu ikihitaji ushindi kwa sababu tofauti. Ni mechi ya kusisimua ambayo haitakiwi kukosa!

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Real Madrid Yaweka Dau la Pauni Milioni 90 Kumnasa Bruno Fernandez
  2. Kagera Sugar Yagonga Mwamba Usajili wa George Mpole
  3. Ratiba ya Nusu Fainali Kombe la FA 2024/2025 England
  4. Timu Zilizofuzu Nusu Fainali Kombe la FA Uingereza 2024/2025
  5. Haaland na Marmoush Waipeleka Man City Nusu Fainali FA Cup
  6. Nyota Wa Real madrid Hatiani Kuikosa Robo fainali UEFA Dhidi ya Arsenal
  7. Timu Zilizofuzu Robo Fainali Kombe la Shirikisho CRDB Federation Cup 2024/2025
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo