Straika wa Mali Amara Bagayoko Atua Coastal Union

Straika wa Mali Amara Bagayoko Atua Coastal Union

Coastal Union imekamilisha uhamisho wa mshambuliaji raia wa Mali, Amara Bagayoko, kutoka klabu ya ASKO de Kara ya Togo. Uhamisho huu unaashiria hatua muhimu katika kuboresha kikosi chao kwa msimu ujao, hasa ikiwa inatarajia kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1989.

Amara Bagayoko, mwenye umri wa miaka 25, alionekana kuwa na kiwango cha hali ya juu msimu uliopita akiwa na ASKO de Kara. Alikuwa mfungaji bora wa Ligi ya Togo baada ya kufunga mabao 19. Pia, Bagayoko amewahi kucheza katika timu mbalimbali za kimataifa ikiwa ni pamoja na FC Nouadhibou ya Mauritania, Al-Hala SC ya Bahrain, na Djoliba AC ya Mali.

Straika wa Mali Amara Bagayoko Atua Coastal Union

Mkataba na Malengo ya Coastal Union

Coastal Union imeingia mkataba wa miaka miwili na mshambuliaji huyu, ikilenga kuimarisha kikosi chao katika michuano ya ndani na kimataifa. Abbas Elsabri, Ofisa Habari na Mawasiliano wa Coastal Union, amesema kuwa malengo yao ni kujenga timu imara itakayoshindana vizuri msimu ujao. Elsabri alisema, “Lengo letu ni kutengeneza timu imara itakayoleta ushindani msimu ujao kwa sababu kama ambavyo unafahamu tuna mashindano ya ndani na ya kimataifa.”

Maandalizi na Mikakati ya Timu

Kuhusu maandalizi ya timu, Coastal Union inafanya kambi kisiwani Pemba huku ikijipanga kwa ajili ya mchezo wao wa nusu fainali ya Ngao ya Jamii dhidi ya Azam FC, utakaopigwa Agosti 8 mwaka huu kwenye Uwanja wa New Amaan Complex Zanzibar. Elsabri alisema, “Kambi yetu itaendelea hapa Pemba hadi siku ya mwisho ya mchezo wetu na Azam FC, hivyo hatuna ratiba ya kurudi jijini Tanga kwa sasa. Kikosi chetu kimejipanga vizuri kuhakikisha kinafanya vizuri licha ya kutambua ugumu uliopo mbele yetu.”

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Khalid Aucho Atwaa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mashabiki wa Yanga
  2. Viingilio Yanga Vs Simba Vita ya Ngao Ya Jamii 2024
  3. Ratiba ya Ngao ya Jamii 2024
  4. Wiki ya Mwananchi 2024 (Yanga Day): Tarehe, Matukio na Bei ya Tiketi
  5. Washindi wa Tuzo za TFF 2023/2024
  6. Tetesi za Usajili simba 2024/2025
  7. Tetesi za Usajili Ligi Kuu Tanzania Bara 2024/2025
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo