Stellenbosch VS Simba SC Leo 27 April 2025 Saa Ngapi?
Wekundu wa Msimbazi, Simba SC, leo watashuka dimbani kuwakabili wenyeji wao Stellenbosch FC katika mchezo wa marudiano wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu wa 2024/2025. Mchezo huu muhimu, ambao utaamua hatma ya kufuzu fainali, utapigwa katika Uwanja wa Moses Mabhida uliopo Durban, Afrika Kusini kuanzia saa 10:00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki (EAT). Simba SC wakiwa na faida ya bao moja walilolipata katika mchezo wa kwanza uliopigwa Zanzibar, wanahitaji kutumia kila nafasi kuhakikisha wanaendeleza mafanikio yao.
Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza ulioimua vumbi katika viunga vya Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar, Simba SC waliibuka na ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Stellenbosch licha ya kupoteza nafasi nyingi za wazi.
Bao hilo lilifungwa na Jean Charles Ahoua dakika ya 45+2 kwa mkwaju wa faulo, likiwapa Simba mtaji muhimu kuelekea mchezo wa marudiano. Hali hiyo inaweka shinikizo kwa Stellenbosch ambao watalazimika kushinda kwa idadi ya mabao zaidi ili kugeuza matokeo.
Kocha Mkuu wa Simba, Fadlu Davids, ameweka wazi mikakati ya timu hiyo kuelekea mchezo wa leo. Katika mahojiano na vyombo vya habari, Davids alieleza kuwa Simba SC hawataingia dimbani kwa kujilinda, bali kwa kushambulia kwa nguvu tangu dakika za awali. Anasisitiza kuwa lengo ni kupata bao la mapema ambalo litawavuruga wapinzani na kuwaweka katika hali ya kutatanika.
Ameongeza kuwa, licha ya kuwa sare yoyote inaweza kuwasogeza Simba hadi fainali, falsafa ya klabu hiyo ni kucheza kwa kutafuta ushindi na si kutegemea matokeo ya kuridhisha. “Tunacheza kushinda, si kutafuta sare. Simba ni klabu kubwa, tunahitaji kutawala mchezo na kuthibitisha ubora wetu,” alisisitiza Davids.
Aidha, alikiri kuwa dakika 10 za mwanzo zitakuwa muhimu sana katika kuelekeza mwelekeo wa mchezo, akitilia mkazo umuhimu wa umakini mkubwa ili kuhakikisha wanafaulu kuanzisha mashambulizi yenye tija.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Mayele Aipeleka Pyramid Fainali Klabu Bingwa Afrika CAF
- Al Ahly Yamtimua Kocha Marcel Koller Baada ya Kutolewa Klabu Bingwa Afrika
- Mtibwa Sugar Yarejea Ligi Kuu NBC 2025/2026
- Timu Zilizofuzu Nusu Fainali Kombe la Muungano 2025
- JKU Yaiondoa Singida Black Stars Kombe la Muungano
- Wachezaji Saba Watimuliwa Zanzibar Kwa Tuhuma Za Kubeti
- Refa Mpya Apangwa Kuongoza Mechi ya Stellenbosch Dhidi ya Simba
Leave a Reply