Stars Kulipa Kisasi Dhidi ya Sudan Leo Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam – Mshindi Kukutana na Ethiopia Raundi ya Pili

Kikosi cha starts vs sudan leo

Stars Kulipa Kisasi Dhidi ya Sudan Leo Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam

Timu ya Taifa ya mpira wa Miguu Tanzania almaarufu kama Taifa Stars leo itakua na kibarua cha kulipiza kisasi dhidi ya Sudani katika mchezo wa marudiano utakaofanyika kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Mchezo huu ni muhimu kwani utaamua hatima ya Stars katika mchakato wa kufuzu kwa Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) 2025, ambazo zitafanyika Kenya, Uganda, na Tanzania.

Katika mchezo wa awali uliofanyika wikiendi iliyopita huko Mauritania, Taifa Stars ilijikuta ikilala kwa bao 1-0 mbele ya Sudan, matokeo ambayo sasa yamezua hamasa kubwa miongoni mwa wachezaji na mashabiki.

Leo, Stars wana fursa adimu ya kulipiza kisasi na kusonga mbele katika raundi ya pili ya michuano, ambako mshindi ataenda kuvaana na Ethiopia, ambao wamepita moja kwa moja baada ya Eritrea kujitoa kwenye mashindano.

Stars Kulipa Kisasi Dhidi ya Sudan Leo Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam – Mshindi Kukutana na Ethiopia Raundi ya Pili

Maandalizi ya Taifa Stars: Kujifua kwa Lengo la Ushindi

Tangu kurejea kutoka Mauritania, Stars imekua ikiendelea na mazoezi makali katika viwanja vya TRA, Kurasini, na KMC Mwenge. Kocha Mkuu Bakar Shime ameeleza kuwa kikosi chake kimejiandaa vyema kukabiliana na Sudan, huku wakitumia mazoezi hayo kutatua mapungufu yaliyoonekana katika mchezo wa awali.

Kocha Shime alisema, “Ni mchezo mgumu na hasa baada ya kupoteza ugenini. Wasudan watakuja wakitaka kulinda ushindi wao, nasi tunataka kulipa kisasi ili tusonge mbele.”

Wachezaji pia wameonyesha kujiamini na morali iko juu. Timu itaendelea kutegemea wachezaji wenye uzoefu wa Ligi Kuu Tanzania na nyota kadhaa kutoka kikosi cha vijana wa U20 waliofanikiwa kubeba ubingwa wa Cecafa.

Uhakika wa Taifa Stars Katika Michuano ya CHAN 2025

Mwaka 2025, Tanzania itaandaa fainali za CHAN sambamba na nchi jirani za Kenya na Uganda, hivyo kuwa mwenyeji kunawapa nafasi ya moja kwa moja kushiriki katika mashindano hayo.

Hata hivyo, Stars hawatumii hili kama sababu ya kubweteka; wanapania kufanya vizuri katika raundi hii ya awali na kujihakikishia ushindi ambao utawapa nguvu zaidi kuelekea michuano ya CHAN na Afcon 2027 ambayo pia itafanyika katika nchi za Afrika Mashariki.v

Changamoto Zinazowakabili Stars Dhidi ya Sudan

Licha ya maandalizi mazuri, Stars wanakutana na changamoto kadhaa. Kwanza, Sudan inatarajiwa kuja na mkakati wa kujihami zaidi, ikilenga kulinda ushindi wao wa awali. Pia, presha ya kushinda mchezo huu inaweza kuwa changamoto, ingawa uwepo wa mashabiki wa nyumbani unaweza kuimarisha ari ya wachezaji wa Taifa Stars.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Kilicho iponza Yanga Dhidi ya Azam Fc
  2. Kikosi cha Azam Fc Vs Yanga SC Leo 02 Novemba 2024
  3. Orodha ya Vinara wa Clean Sheets Ulaya
  4. Simba Yabeba Pointi Tatu kwa Mbinde Dhidi ya Mashujaa
  5. Ratiba ya Mechi za Leo Ligi Kuu ya NBC Tanzania 02/11/2024
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo