Singida Black Stars Yawatumbua Makocha Aussems na Kitambi!

Singida Black Stars Yawatumbua Makocha Aussems na Kitambi

Singida Black Stars Yawatumbua Makocha Aussems na Kitambi!

Klabu ya Singida Black Stars imewasimamisha makocha wake wawili, Patrick Aussems na msaidizi wake Dennis Kitambi, kufuatia mfululizo wa matokeo yasiyoridhisha kwenye mechi za hivi karibuni. Hatua hii imekuja wakati taarifa zikihusisha timu hiyo na kocha wa zamani wa Yanga, Miguel Gamondi, kama mbadala wa Aussems.

Hatua ya kusimamishwa kwa Aussems na Kitambi ilitangazwa kupitia taarifa rasmi ya klabu tarehe 25 Novemba 2025. Uamuzi huu ulifikiwa na Bodi ya Ukurugenzi ya Singida Black Stars kufuatia mwenendo wa timu kushindwa kufikia matarajio, ikipoteza mchezo mmoja na kutoka sare mara mbili mfululizo.

“Bodi ya Ukurugenzi ya Singida Black Stars imefikia uamuzi wa kuwasimamisha kazi makocha Patrick Aussems pamoja na Denis Kitambi kutokana na mwenendo usioridhisha wa timu,” ilisema taarifa hiyo rasmi.

Kwa sasa, timu iko chini ya Mkurugenzi wa Ufundi Ramadhani Nsanzurwimo kama kocha mkuu wa muda, akisaidiwa na Muhibu Kanu.

Singida Black Stars Yawatumbua Makocha Aussems na Kitambi!

Matokeo ya Hivi Karibuni

Singida Black Stars walilazimishwa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Tabora United katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Al Hassan Mwinyi. Sare hiyo ilikuwa ya tatu mfululizo kwa klabu hiyo, ambayo kwa sasa inashikilia nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara. Licha ya kuwa na pointi 24 sawa na Yanga na Azam, mwenendo wa timu haujalingana na matarajio ya uongozi na mashabiki wake.

Katika michezo 11 iliyopita, Singida Black Stars imeshinda mechi saba, kutoka sare mbili, na kupoteza moja dhidi ya Yanga SC. Timu imefunga mabao 15 huku ikiruhusu sita.

Gamondi Katika Majadiliano

Taarifa zilizopo inasemekana kuwa Singida Black Stars inamfikiria kocha Miguel Gamondi, ambaye hivi karibuni alitangazwa kuenguliwa katika nafasi yake kama Kocha wa Yanga SC. Gamondi, aliyeipa Yanga ubingwa wa Ligi Kuu msimu uliopita, aliondolewa kutokana na ukosefu wa ushindi kwenye mechi tatu mfululizo, licha ya mafanikio yake makubwa. Mashabiki wa Singida wananekana kuunga mkono uwezekano wa kumleta Gamondi, huku wakimwona kama chaguo bora la kuleta mafanikio ya haraka.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Matokeo ya Yanga vs Al Hilal leo 26/11/2024
  2. Ratiba ya yanga Klabu Bingwa CAF 2024/2025
  3. Ratiba ya Makundi Klabu Bingwa CAF 2024/2025
  4. Msimamo wa Kundi la Yanga Klabu Bingwa Afrika CAF 2024/2025
  5. Kikosi cha Yanga vs Al Hilal leo 26/11/2024
  6. Rekodi za Refa Atakaye Chezesha Mechi ya Yanga vs Al Hilal
  7. Ratiba ya Mechi za leo 26/11/2024
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo