Simba Yakwama Kumsajili Okello, Vipers Wachomoa Betri

Simba Yakwama Kumsajili Okello

Simba Yakwama Kumsajili Okello, Vipers Wachomoa Betri

Juhudi za wekundu wa Msimbazi za kunasa saini ya kiungo mahiri wa Vipers SC, Allan Okello, zimeshindikana baada ya mabingwa hao wa Uganda kuweka msimamo wa kutomuachia nyota wao huyo. Hii si mara ya kwanza kwa Vipers kukwamisha ndoto za Simba, kwani awali walizuia uhamisho wa straika wao Cesar Lobi Manzoki, ambaye baadaye alihamia China.

Kwa muda mrefu, Simba ilikuwa ikiwania huduma za Okello ili kuongeza nguvu katika eneo la kiungo kabla ya kufungwa kwa dirisha dogo la usajili. Hata hivyo, juhudi hizo zimegonga mwamba, kwani Vipers imeweka wazi kuwa mchezaji huyo ni muhimu kwa mipango yao.

Nyota huyo wa Uganda, ambaye ana uwezo wa kucheza nafasi mbalimbali za kiungo, alikuwa tegemeo kwa Vipers msimu huu. Kwa sasa, timu hiyo inashikilia nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu ya Uganda huku Okello akiwa na mabao nane, bao moja nyuma ya kinara wa ufungaji, Ivan Ahimbisibwe wa URA SC.

Simba Yakwama Kumsajili Okello, Vipers Wachomoa Betri

Sababu za Kufeli kwa Dili

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya Vipers, sababu kubwa ya kugomea uhamisho wa Okello ni kutaka kumtumia kwenye Fainali za Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) 2025, zitakazofanyika Uganda, Tanzania, na Kenya. Vipers imeeleza kuwa Okello ni muhimu si tu kwa klabu yao bali pia kwa timu ya taifa ya Uganda, na hawako tayari kuhatarisha nafasi yao kwa kumruhusu kuondoka.

Pia, Rais wa Vipers, Lawrence Mulindwa, ameonekana kuwa kikwazo kikubwa katika uhamisho huo. Historia inaonyesha kuwa Mulindwa huwa hana haraka ya kuuza wachezaji wake muhimu, hasa wanapokuwa bado wanahitajika na timu. Hali hii ilishuhudiwa pia wakati wa kisa cha Manzoki, ambaye alihamishwa baada ya klabu kufanikisha mpango wa kumpeleka China.

Simba Watafuta Mbadala

Kwa sasa, Simba imelazimika kuachana rasmi na mpango wa kumsajili Okello na kuanza kutafuta kiungo mwingine ambaye ataweza kuongeza nguvu kwenye kikosi. Lengo kuu la Simba ni kuhakikisha wanajihakikishia ubora wa kutetea taji lao la Ligi Kuu ya NBC pamoja na kufanya vizuri kwenye michuano ya kimataifa.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Fadlu Akabidhi Faili usajili Dirisha Dogo
  2. Simba Yaamishia Majeshi ya Usajili Kwa Fei Toto Baada ya Mpanzu
  3. Msimamo wa Kundi la Yanga Klabu Bingwa Afrika CAF 2024/2025
  4. Matokeo ya Al Hilal VS Yanga Leo 12/01/2025
  5. Timu Zilizofuzu Robo Fainali Kombe La Shirikisho Afrika 2024/2025
  6. Msimamo Kundi la Simba Kombe la Shirikisho CAF 2024/2025
  7. Matokeo ya Bravos do Maquis vs Simba SC Leo 12/01/2025
  8. Timu Zilizofuzu Robo Fainali Klabu Bingwa Afrika 2024/2025
  9. Rachid Taoussi Apania Kushusha Nyota Zaidi Dirisha Dogo
  10. AS Vita Yamnyakua Dennis Modzaka Kutoka Coastal Union
  11. Rabbin Sanga Ajiunga na Tanzania Prisons Kwa Mkopo
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo