Simba Yajizolea Ponti tatu Muhimu Kwa Pamba Jiji

Simba vs pamba jiji

Simba Yajizolea Ponti tatu Muhimu Kwa Pamba Jiji

Wekundu wa Msimbazi Simba jana wameendeleza ubabe katika mechi za ugenini za Ligi Kuu msimu huu, wakizidi kujichimbia kileleni mwa msimamo wa ligi. Simba walipata ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Pamba Jiji kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza, ushindi ambao unathibitisha dhamira yao ya kutwaa ubingwa msimu huu.

Ushindi huu wa Simba ni wa tano mfululizo katika mechi za ugenini za Ligi Kuu, baada ya kuzifunga Azam, Dodoma Jiji, Tanzania Prisons, na Mashujaa FC. Matokeo haya yanaifanya Simba kufikisha jumla ya pointi 28, na kuendelea kutamba kileleni mwa msimamo wa ligi.

Simba Yajizolea Ponti tatu Muhimu Kwa Pamba Jiji

Bao pekee la mechi hiyo lilifungwa na Lionel Ateba kwa mkwaju wa penalti dakika ya 23, penalti iliyotolewa baada ya beki wa Pamba, Christopher Oruchum, kumchezea rafu Ateba ndani ya eneo la hatari. Ushindi huu ulikuwa muhimu kwa Simba, huku Ateba akivunja ukame wa mabao ulioendelea kwa mechi saba mfululizo.

Mechi hiyo haikutoa fursa kubwa kwa wachezaji kuonyesha vipaji vyao kutokana na hali ya uwanja wa CCM Kirumba kuwa na unyevu, pengine kutokana na mvua zilizonyesha Mwanza siku za hivi karibuni. Hali hiyo ilizilazimisha timu zote kutumia mipira mirefu mara kwa mara, huku pasi za haraka zikionekana kuwa ngumu kutekelezeka.

Mwamuzi Hussein Katanga alikumbana na malalamiko kutoka kwa wachezaji wa Pamba mara baada ya kipindi cha kwanza, hasa kutokana na uamuzi wake wa kutomuonyesha kadi nyekundu Shomari Kapombe wa Simba kwa faulo aliyomfanyia George Mpole wa Pamba.

Ingawa Mpole alikuwa akielekea moja kwa moja langoni, uwepo wa beki mwingine wa Simba, Chamou Karaboue, huenda ulisababisha mwamuzi kuamua kuwa haikuwa nafasi ya wazi ya kufunga bao.

Kipindi cha pili kilishuhudia timu zote zikifanya mabadiliko muhimu. Pamba Jiji FC walimtoa Paulin Kasindi na kumuingiza Alain Mukeya, huku Simba wakimpumzisha Charles Ahoua kwa Kibu Denis. Simba pia walifanya mabadiliko ya mara kwa mara, lakini ni Pamba walioonekana kutawala mchezo kwa muda mwingi wa kipindi cha pili.

Licha ya jitihada zao, ukosefu wa umakini wa kutumia nafasi walizopata uliwanyima Pamba nafasi ya kusawazisha bao. Kipa wa Simba, Moussa Camara, alionyesha uwezo mkubwa kwa kuokoa mashuti kadhaa ya hatari, likiwemo shuti la dakika ya 60 kutoka kwa James Mwashinga na nafasi ya dakika ya 81 ya Samuel Antwi.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Ratiba ya Mechi za Leo 23/10/2024 Ligi Kuu NBC
  2. Matokeo ya Pamba Jiji VS Simba Sc Leo 22/11/2024
  3. Fadlu Akabidhi Faili usajili Dirisha Dogo
  4. Kikosi Cha Simba Sc VS Pamba Jiji Leo 22/11/2024
  5. Moallin ajipanga kuipaisha Yanga
  6. Prisons Yajipanga Kuvuna Pointi dhidi ya JKT
  7. Simba SC Yalaani Kitendo Cha Polisi Kuingilia Mazoezi Kirumba
  8. Viingilio Mechi ya Pamba jiji Vs Simba Sc Leo 22/11/2024
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo