Simba Yafungua Michuano ya Makundi ya CAF kwa Ushindi wa 1-0
Wekundu wa Msimbazi, Simba SC, wameanza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho la TotalEnergies CAF kwa ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Bravos do Maquis ya Angola katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
Ushindi huu mwembamba ulihitimishwa na penalti ya Jean Ahoua katika kipindi cha kwanza, ikiwapa Simba SC alama tatu muhimu na kuwaweka kileleni mwa Kundi A baada ya mechi ya kwanza.
Penati iliozaa goli za Simba ilipatikana katika dakika ya 27 ya mchezo, Simba walipata nafasi ya dhahabu baada ya mchezaji wa Bravos, Edmilson, kushika mpira ndani ya eneo la hatari.
Penalti hiyo ilipigwa kwa ustadi mkubwa na Jean Ahoua, ambaye aliupiga mpira kwa ustadi kuelekea kona ya juu kushoto, bila kumpa nafasi kipa wa Bravos. Goli hili lilikuwa la kipekee katika mchezo huu uliokuwa na ushindani mkubwa.
Huku wakiongozwa na kocha mpya, Davids, Simba walionekana kuimarika zaidi katika sehemu ya kwanza ya mchezo. Steven Mukwala alikaribia kuongeza bao mara kadhaa lakini alikosa bahati katika harakati zake.
Kipindi cha pili cha mchezo kilianza kwa kasi, huku Bravos do Maquis wakijaribu kusawazisha. Dakika ya 48, timu hiyo ya Angola ilipata penalti, lakini juhudi za Emmanuel Edmond ziliangukia pua baada ya kipa wa Simba kuokoa mpira huo kwa umahiri mkubwa.
Bravos walionyesha dalili za kuweza kusawazisha kupitia wachezaji wao mahiri kama Jó Paciência na Macaiabo, lakini mashuti yao yalizuiwa au kuishia nje ya lango. Kwa upande mwingine, Simba walikaribia kuongeza bao la pili kupitia Joshua Mutale, ambaye shuti lake dakika ya 66 liligonga mwamba.
Msimamo wa Kundi A Baada ya Mechi ya Kwanza
- Simba SC (Tanzania): Pointi 3
- CS Sfaxien (Tunisia): Pointi 0 (bado haijacheza)
- Constantine (Algeria): Pointi 0 (bado haijacheza)
- Bravos do Maquis (Angola): Pointi 0
Mapendekezo ya Mhariri;
- Matokeo ya Simba vs FC Bravos do Maquis leo 27/11/2024
- Kikosi cha Simba vs FC Bravos do Maquis leo 27/11/2024
- Sababu 10 za 1xBet Kuwa Kipenzi Cha Watanzania Wengi
- Msuva Asubiri Mkataba Mpya Mnono Al-Talaba SC
- Kocha Kagera amsifu Charles Boniface Mkwasa: ‘Kocha bora nchini’
- Msimamo Kundi la Simba Kombe la Shirikisho CAF 2024/2025
Leave a Reply