Simba VS Tanzania Prisons Leo 11/02/2024 Saa Ngapi?

Simba VS Tanzania Prisons Leo 11 02 2024 Saa Ngapi

Simba VS Tanzania Prisons Leo 11/02/2024 Saa Ngapi?

Wekundu wa Msimbazi, Simba SC, leo watashuka dimbani kuvaana na Wajelajela, Tanzania Prisons, katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara. Mchezo huu unatarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa KMC Complex, Dar es Salaam, kuanzia saa 10:00 jioni. Ni mechi muhimu kwa timu zote mbili, zikiwa na malengo tofauti lakini muhimu katika msimamo wa ligi.

Simba VS Tanzania Prisons Leo 11/02/2024 Saa Ngapi?

Simba SC: Kutafuta Ushindi Baada ya Sare

Kocha wa Simba, Fadlu Davids, ana mtihani wa kurekebisha makosa yaliyojitokeza kwenye mechi yao iliyopita dhidi ya Fountain Gate, ambapo walipata sare ya 1-1 ugenini. Matokeo hayo yalisitisha rekodi nzuri ya ushindi wa mechi nane mfululizo ugenini kwa Simba.

Licha ya changamoto hiyo, Simba inajivunia rekodi nzuri nyumbani msimu huu, ambapo imeshinda mechi sita kati ya nane zilizopita, ikipoteza moja na kutoka sare mara moja.

Fadlu amesisitiza umuhimu wa kushambulia kwa kasi na kuhakikisha wanapata bao la mapema ili kuwavuruga wapinzani wao. “Tutaendelea na mtindo wetu wa kutengeneza nafasi nyingi na kufunga mabao mapema ili kuondoa presha kwa wachezaji wetu na kuwafanya wapinzani kupoteza kujiamini,” alisema Fadlu.

Tanzania Prisons: Kuendeleza Rekodi Nzuri Duru la Pili

Tanzania Prisons inaingia kwenye mchezo huu ikiwa na mwendelezo mzuri baada ya kushinda mechi mbili mfululizo dhidi ya Pamba Jiji (1-0) na Mashujaa FC (2-1). Kikosi hiki kinachonolewa na Kocha Amani Josiah kimepata mwamko mpya tangu alipochukua mikoba ya Mbwana Makata Desemba 28, 2024.

Prisons inatafuta kulipa kisasi baada ya kupoteza mchezo wa duru la kwanza dhidi ya Simba kwa bao 1-0 nyumbani. Timu hii kwa sasa ipo katika nafasi ya 14 kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 17 baada ya michezo 17, hali inayowafanya kupambana vikali ili kujiondoa katika hatari ya kushuka daraja.

Kocha Josiah amesisitiza kuwa hana presha kubwa kwa wachezaji wake na anawataka wafurahie mchezo. “Siwezi kuwapa wachezaji wangu shinikizo la kushinda dhidi ya Simba, lakini ninaamini kuwa naweza kutumia mbinu sahihi kupunguza udhibiti wao wa mpira na kutumia vyema nafasi zetu,” alisema Josiah.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. YANGA warejea nyumbani na pointi moja baada ya sare na JKT Tanzania
  2. Matokeo ya JKT Tanzania Vs Yanga Leo 10/02/2025
  3. Kikosi cha Yanga vs JKT Tanzania Leo 10/02/2025
  4. Ratiba ya Mechi za Leo 10 Februari 2025
  5. Viingilio Mechi ya JKT Tanzania Vs Yanga Leo 10/02/2025
  6. JKT Tanzania Vs Yanga Leo 10/02/2025 Saa Ngapi?
  7. Bao la Kaseke Laipa Pamba Ushindi Dhidi ya Azam FC
  8. Ushindi Dhidi ya Dodoma Jiji Wampa Jeuri Minziro
  9. Ngassa: Mechi dhidi ya Simba itakuwa ngumu, lakini tunajua pakupenya
  10. KenGold Yaahidi Kujifuta Machozi ya 6-1 Mbele ya Fountain Gate
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo