Simba VS CS Sfaxien Leo 15/12/2024 Saa Ngapi?
UKISIKI Jumapili maalumu, basi ndiyo leo! Hii ni Jumapili ya soka yenye vipute vya maana vitakavyochezwa kutoka Tanzania hadi Ulaya na Afrika. Kama wewe ni shabiki wa soka, basi leo ni siku ya kufurahia mechi kubwa kuanzia saa 10 jioni hadi usiku wa manane.
Usikose mechi ya kibabe itakayochezwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, ambapo Mnyama Simba atakuwa akicheza dhidi ya CS Sfaxien ya Tunisia katika mechi muhimu ya Kombe la Shirikisho la Afrika.
Mda wa Mechi ya Simba Vs CS Sfaxien
Mechi kati ya wekundu wa msimbazi Simba SC na CS Sfaxien leo tarehe 15 Desemba 2024 itapigwa kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, kuanzia saa 10:00 jioni. Hii ni mechi muhimu kwa Simba, ambao wanapigania kujieka katika nafasi nzuri itakayo wawezesha kutimiza ndoto yao ya kusonga mbele katika hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho la Afrika.
Mashabiki wa soka kote nchini na Afrika wanatarajia mchezo wa wenye mvuto wa kipekee, kwani timu zote mbili zina historia nzuri katika mashindano ya CAF. Hata hivyo, Simba wanapewa nafasi kubwa kutokana na rekodi yao bora ya nyumbani, huku mashabiki wa Msimbazi wakitarajiwa kujitokeza kwa wingi kuipa nguvu timu yao.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Jackson Shiga Anukia Fountain Gate
- Bao la Mwisho la Dube Laipa Yanga Point dhidi ya TP Mazembe
- Msimamo wa Kundi la Yanga Klabu Bingwa Afrika CAF 2024/2025
- Matokeo ya Tp Mazembe VS Yanga Leo 14/12/2024
- Kikosi cha Yanga vs Tp Mazembe Leo 14/12/2024
- Yanga vs Tp Mazembe Leo 14/12/2024 Saa Ngapi?
- Miguel Cardoso Akabidhiwa Mikoba ya Ukocha Mamelodi
Leave a Reply