Simba SC Yalaani Kitendo Cha Polisi Kuingilia Mazoezi Kirumba

Simba SC Yalaani Kitendo Cha Polisi Kuingilia Mazoezi Kirumba

Simba SC Yalaani Kitendo Cha Polisi Kuingilia Mazoezi Kirumba

Klabu ya Simba SC imelaani vikali matumizi ya vyombo vya dola, hususan Polisi, kuingilia mazoezi yao katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, ikiwa ni maandalizi ya mechi yao dhidi ya Pamba FC. Tukio hili, lililotokea Novemba 21, 2024, limeibua mjadala mkubwa katika medani ya soka nchini, huku Simba ikieleza masikitiko yake juu ya matumizi ya nguvu na usumbufu uliosababishwa.

Tukio Lilivyotokea

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa uongozi wa Simba SC, klabu hiyo ilikuwa imepanga kufanya mazoezi ya mwisho kabla ya mchezo wao dhidi ya Pamba FC kwenye uwanja wa CCM Kirumba, Novemba 22, 2024. Hata hivyo, wakati timu hiyo ilipofika uwanjani kwa ajili ya mazoezi, viongozi wa timu ya Pamba walizuia mazoezi hayo kutekelezwa.

Licha ya jitihada za viongozi wa Simba SC kuwasihi wachezaji wa Pamba kuondoka uwanjani ili kuwaruhusu kufanya mazoezi yao, hali hiyo ilizidi kuzidi, na Pamba waligusha hali hiyo kwa kujifungia kwenye chumba cha mikutano cha uwanja huo.

Hali ilizidi kuwa ya kushangaza wakati Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mh Said Mtanda, alifika uwanjani akiwa na maafisa wa Polisi, baadhi wakiwa na silaha. Polisi walikataa kutoa maelezo ya msingi kuhusu sababu za wao kuingia uwanjani na kuingilia shughuli  za Simba SC.

Simba SC Yatoa Tamko

Simba SC kupitia taarifa yao kwa umma, imelalamikia matumizi ya nguvu katika tukio hilo na kudai kuwa hali hiyo ni njama za kudhoofisha maandalizi ya timu kuelekea mchezo muhimu dhidi ya Pamba FC. Klabu hiyo imekemea vikali vitendo vya viongozi wa soka kutumia vyombo vya dola vibaya, huku wakitoa wito kwa mamlaka husika kuhakikisha sheria na kanuni za mchezo zinaheshimiwa.

Taarifa hiyo ilisema: “Tunalaani matumizi ya nguvu yaliyotumika katika sakata hili na kuwakamata maafisa wa klabu yetu bila ya sababu za msingi. Tukio hili linaashiria jitihada za kudhoofisha timu yetu kuelekea mchezo wa kesho. Tunawasisitiza viongozi wenye mamlaka kutumia nafasi zao kwa njia sahihi na yenye maadili.”

Simba SC Yalaani Kitendo Cha Polisi Kuingilia Mazoezi Kirumba

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Viingilio Mechi ya Pamba jiji Vs Simba Sc Leo 22/11/2024
  2. Matokeo ya Pamba Jiji VS Simba Sc Leo 22/11/2024
  3. Kikosi Cha Simba Sc VS Pamba Jiji Leo 22/11/2024
  4. Pamba Jiji vs Simba Sc Leo 22/11/2024 Saa Ngapi?
  5. Fadlu Davids Aelezea Mikakati Ya Simba Kuelekea Mechi Ya Pamba Jiji
  6. Morrison Atema Cheche Ghana kushindwa kufuzu Afcon 2025
  7. Ushindi dhidi ya Yanga Waipa Tabora United Mzuka wa Kuwachapa Singida
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo