Simba Queens Kuachana na Yussif Basigi Mwisho wa Msimu

Simba Queens Kuachana na Yussif Basigi Mwisho wa Msimu

Simba Queens Kuachana na Yussif Basigi Mwisho wa Msimu

Simba Queens inajiandaa kuachana rasmi na Kocha Mkuu wao, Yussif Basigi, mara baada ya msimu huu wa Ligi Kuu ya Wanawake kumalizika, kutokana na kutoridhisha kwa mwenendo wa timu chini ya uongozi wake. Hili linaelezwa kuwa ni hatua ya kimkakati baada ya viongozi wa klabu hiyo kutathmini matokeo ya msimu na kubaini kwamba matarajio waliyojiwekea hayajatimizwa kikamilifu.

Basigi alijiunga na Simba Queens mwanzoni mwa msimu huu akitokea Hasacaas Ladies ya Ghana. Akiwa kwenye msimu wake wa kwanza kabisa katika Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara, amefanikisha ushindi katika mechi 12, huku akipoteza mchezo mmoja dhidi ya Yanga Princess na kutoka sare mmoja na JKT Queens.

Simba Queens Kuachana na Yussif Basigi Mwisho wa Msimu

Hata hivyo, pamoja na matokeo hayo ya jumla kuwa mazuri kwenye karatasi, viongozi wa Simba Queens wanaripotiwa kuwa na mashaka juu ya uwezo wa Basigi kufikia malengo ya klabu hiyo, hususan kutwaa mataji yote makubwa, kama walivyofanya msimu uliopita chini ya aliyekuwa kocha Juma Mgunda. Mgunda aliongoza Simba kutwaa ubingwa wa ligi bila kupoteza mchezo wowote, huku akiifunga Yanga Princess na JKT Queens, nyumbani na ugenini, kabla ya kujiunga na Namungo FC.

Kwa mujibu wa taarifa zilizothibitishwa na chanzo cha habari ndani ya klabu hiyo, uongozi wa Simba tayari umefikia uamuzi wa kutompa mkataba mpya Basigi, ambaye awali alisaini mkataba wa mwaka mmoja pekee. Mpango ni kumruhusu amalize mechi nne zilizobaki za ligi kabla ya kuachana naye rasmi mwishoni mwa msimu.

Chanzo hicho kilieleza kuwa uongozi wa timu ulifanya majadiliano ya kina na kufikia hitimisho kwamba kocha huyo hana uwezo wa kufikia matarajio waliyojiwekea tangu msimu unaanza. Malengo hayo yalijumuisha pia kutwaa Kombe la Ngao ya Jamii, ambalo lilienda kwa JKT Queens.

“Ligi bado inaendelea lakini kwa inavyoonekana kuna uwezekano hata ubingwa wa ligi tukaukosa. Viongozi tumeshauriana na kuona hakuna haja ya kuendelea naye, tusubiri tu amalize mkataba wake,” kilisema chanzo hicho.

Viongozi wa Simba Queens walipoteza imani na Basigi tangu walipoibuka na ushindi mwembamba dhidi ya Ceasiaa Queens, ambapo bao pekee lilifungwa katika dakika za mwisho za mchezo. Hapo ndipo walimuita kocha uwanjani na kumhoji kuhusu hali ya kikosi, lakini majibu yake hayakuridhisha.

“Tuligundua shida tangu mechi na Ceasiaa tuliyopata bao moja dakika za jioni, tulimwita kocha pale pale uwanjani na kumuuliza kama kuna shida sehemu, akajibu hakuna. Kwa hiyo maamuzi ni hayo,” alieleza zaidi mtoa taarifa.

Kwa kuzingatia mwenendo huu, wadau wa soka wanashauri klabu kuwa na utulivu katika kipindi hiki cha mpito na kufanya tathmini ya kina kabla ya kumleta kocha mpya. Aidha, inaleta picha wazi kuwa mafanikio ya kihistoria ya Simba Queens yameweka kiwango cha juu cha matarajio, hali inayomlazimu kila kocha mpya kuleta matokeo ya haraka.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Rupia Atupia Goli lake la 10 na Kuipa Singida Big Stars Pointi 3 Muhimu Dhidi ya Azam FC
  2. Man United Walazimishwa Sare na Man City Nyumbani Old Trafford
  3. Prince Dube Afukuzia Rekodi Yake Yanga Kimya Kimya
  4. PSG Yatwaa Ubingwa Ligi Kuu Ufaransa 2024/2025 Huku wakiwa Bado na Michezo 6
  5. Mambo Bado Yamoto Ligi Kuu Tanzania
  6. Yanga Yaingia Mawindondi Kuisaka Saini ya Mohamed Omar Ali
  7. Fei Toto Aelezea Umuhimu wa Mechi Sita Zilizosalia Kwa Azam
  8. De Bruyne Atangaza Kuondoka Man city Mwishoni Mwa Msimu
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo