Simba na Yanga Zaekwa Kiporo Ratiba Mpya ya Kombe la FA
SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetoa ratiba kamili ya raundi ya tatu ya Kombe la FA huku klabu kubwa za Simba SC na Yanga SC zikiwa hazijapangiwa tarehe za michezo yao kutokana na kushiriki kwenye michuano ya kimataifa.
Kwa mujibu wa ratiba hiyo, michezo ya raundi ya tatu ya Kombe la FA inatarajiwa kuanza Desemba 5 na kuendelea hadi Desemba 8 mwaka huu. Hata hivyo, mashabiki wa Simba na Yanga watalazimika kusubiri tarehe mpya za michezo yao, kwani klabu hizo zinajiandaa kwa mechi muhimu katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho Afrika.
Yanga SC itasafiri hadi Algeria kucheza na MC Alger katika Uwanja wa Julliet wa Tano mnamo Desemba 7, 2024, kwenye mchezo wa kundi A wa Ligi ya Mabingwa Afrika. Mechi hiyo itachezwa saa 4:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.
Kwa upande mwingine, Simba SC itacheza na CS Constantine ya Algeria katika Uwanja wa Mohamed Hamlaoui mnamo Desemba 8, saa 1:00 usiku, ikiwa ni sehemu ya mechi za kundi A za Kombe la Shirikisho Afrika.
Kwa sababu ya ratiba hizo, michezo yao ya raundi ya tatu ya Kombe la FA imeahirishwa. Yanga ilitarajiwa kucheza dhidi ya Copco FC, huku Simba ikipangiwa kucheza na Kilimanjaro Wonders Sports Center. TFF imethibitisha kuwa tarehe mpya za michezo hii zitatangazwa baadaye.
Michezo Mingine ya Raundi ya Tatu ya FA
Ingawa Simba na Yanga hazitashiriki raundi hii kwa sasa, ratiba inaendelea na michezo mingine kama ifuatavyo:
Desemba 7, 2024
- Azam FC vs Iringa Sports – Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
- Singida Big Stars vs Magnet FC – Uwanja wa Liti, Singida.
- Mashujaa FC vs Tukuyu Stars – Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma.
- KMC vs Black Six – Uwanja wa KMC, Kinondoni.
- Fountain Gate vs Mweta Sports – Uwanja wa Tanzanite Kwaraa, Babati.
- Coastal Union vs Stand United – Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.
- Kagera Sugar vs Rhino Rangers – Uwanja wa Kaitaba, Bukoba.
- Dodoma Jiji vs Leo Tena – Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.
Desemba 8, 2024
- Geita Gold vs Ruvu Shooting – Uwanja wa Nyankumbu, Geita.
- Prisons vs Tandika United – Uwanja wa Sokoine, Mbeya.
- JKT Tanzania vs Igunga United – Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Mbweni, Dar es Salaam.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Yanga Yapania Kurejea Kwa Kasi ya kimbunga Ligi Kuu
- Luhende Aonya Mastaa wa Soka Kuhusu Starehe Kupita Kiasi
- Mapambano Makali Yanaendelea Championship 2024/2025
- Tanzania Yapanda kwa kasi katika Viwango vya FIFA
- Leicester kumrudisha Ruud van Nistelrooy EPL
- Yanga Kukabiliwa na Kazi Ngumu ya Kupindua Meza CAF
- Azam FC Yaibuka na Ushindi wa 2-1 dhidi ya Singida Black Stars
Leave a Reply