Sifa za Kujiunga na Jeshi La Polisi Tanzania 2024

Hizi ndizo Sifa za Kujiunga na Jeshi La Polisi Tanzania 2024

Jeshi la Polisi Tanzania ni miongoni mwa nguzo muhimu katika kudumisha amani, usalama, na utulivu nchini. Ili kutimiza wajibu huu mkubwa, Jeshi la Polisi huhitaji kuajiri vijana wenye sifa, ari, na uzalendo wa hali ya juu watakao fanikisha nia na malengo ya jeshi.

Kwa mwaka 2024 Jeshi la polisi limefungua mfumo wa kupokea maombi mapya ya ajira kwa vijana wa Kitanzania wenye ndoto ya kutumikia nchi yao kupitia Jeshi la Polisi.

Lakini, swali kubwa ni je, unazifahamu sifa zinazohitajika ili kujiunga na Jeshi la Polisi Tanzania? Kama hapa basi ungana nasi katika chapisho hili ili kuju a ni vigezo gani huitajika ili kujiunga na jeshi la poilis.

Hapa tutakupa mwanga wa kutosha kuhusu vigezo na sifa za zote za kielimu, maumbile na nyenginezo maalum, mchakato wa kuomba, na vidokezo vya kukusaidia katika safari yako ya kuwa askari polisi nchini Tanzania.

Endelea kusoma ili kujua kama una sifa na jinsi ya kuzitumia kutimiza ndoto yako ya kuvaa sare ya jeshi la polisi Tanzania.

Sifa za Kujiunga na Jeshi La Polisi Tanzania 2024

Sifa za Kujiunga na Jeshi La Polisi Tanzania 2024

Ili kujiunga na Jeshi la Polisi Tanzania mwaka 2024, mwombaji anatakiwa kutimiza sifa zifuatazo:

  1. Mwombaji awe raia wa Tanzania kwa kuzaliwa, mwenye umri kati ya miaka 18 na 25 kwa waombaji wa kidato cha nne, sita, na astashahada, au kati ya miaka 18 na 30 kwa waombaji wa shahada na stashahada.
  2. Waombaji wa kidato cha nne wawe wamehitimu kuanzia mwaka 2018 hadi 2023 na wawe na daraja la I hadi IV, wenye daraja la IV wawe na alama 26 hadi 28.
  3. Waombaji wa kidato cha sita wawe wamehitimu kuanzia mwaka 2018 hadi 2023 na wawe na daraja la I hadi III.
  4. Waombaji wa astashahada, stashahada, na shahada wawe wamehitimu katika fani zinazohitajika na Jeshi la Polisi.
  5. Wanaume wawe na urefu usiopungua futi 5 na inchi 8, wanawake wawe na urefu usiopungua futi 5 na inchi 4.
  6. Mwombaji awe na kitambulisho cha taifa au namba ya utambulisho kutoka NIDA. Awe na uwezo wa kuwasiliana kwa ufasaha katika lugha ya Kiswahili na Kiingereza. Pia, anatakiwa kuwa na afya njema ya kimwili na kiakili, iliyothibitishwa na daktari wa serikali.
  7. Aidha, mwombaji anatakiwa awe hajaoa/kuolewa na hana mtoto. Ni sharti pia kwamba hajawahi kutumia dawa za kulevya na yuko tayari kuhudhuria mafunzo ya awali ya taaluma ya polisi.
  8. Mwombaji hapaswi kuwa ameajiriwa na taasisi yoyote ya serikali. Zaidi ya hayo, anatakiwa kuwa tayari kufanya kazi za polisi popote nchini Tanzania, kujigharamia katika hatua zote za usaili, asiwe na alama za kuchorwa mwilini, na asiwe na kumbukumbu za uhalifu.

Mchakato wa Kutuma Maombi ya Kazi Jeshi la Polisi

Ili kuomba nafasi za kazi kujiunga na Jeshi la Polisi Tanzania, fuata maelekezo yafuatayo hapa chini.

Andika barua ya maombi

Mwombaji anatakiwa kuandika barua ya maombi kwa mkono wake mwenyewe (handwriting). Katika barua, ni muhimu kuhakikisha kuwa namba za simu za mwombaji zimeandikwa kwa usahihi. Barua hii itumwe kwa anuani ifuatayo:

Mkuu wa Jeshi la Polisi
S.L.P 961
DODOMA

Omba kupitia mfumo wa mtandaoni

Baada ya kutuma barua ya maombi, mwombaji anatakiwa kuwasilisha maombi yake kupitia mfumo wa ajira wa Polisi (TANZANIA POLICE FORCE – RECRUITMENT PORTAL). Mfumo huu unapatikana kwenye tovuti rasmi ya Jeshi la Polisi: ajira.tpf.go.tz

Ni muhimu kuzingatia kwamba hatua zote mbili, yaani kutuma barua ya maombi na kuomba kupitia mfumo wa mtandaoni, ni lazima zifuatwe ili maombi ya mwombaji yaweze kuzingatiwa.

Mapendekezo Ya Mhariri:

  1. Muda wa Kutuma Maombi Nafasi za Kazi Jeshi la Polisi Waongezwa
  2. Nafasi Mpya Za Kazi Chuo Kikuu cha SUA: Mwisho wa Kutuma Maombi ni 19 Mei 2024
  3. Vigezo & Sifa za Kujiunga JKT Mujibu Wa Sheria 2024
  4. Orodha Ya Vyuo Bora Tanzania 2024
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo