Serengeti Girls Waibuka Mabingwa Kombe la UNAF U17 Tunisia 2024

Serengeti Girls Waibuka Mabingwa Kombe la UNAF U17 Tunisia 2024

Timu ya taifa ya wasichana ya Tanzania chini ya umri wa miaka 17, maarufu kama Serengeti Girls, imeibuka kuwa mabingwa wa mashindano ya Kombe la UNAF U17 mwaka 2024 yaliyofanyika nchini Tunisia.

Serengeti Girls walionesha uwezo mkubwa wa kiufundi na ushindani wa hali ya juu dhidi ya wapinzani wao kutoka kanda ya Afrika Kaskazini, hatua iliyowafanya kutwaa ubingwa baada ya mechi tatu ngumu za mashindano hayo.

Katika mchezo wa mwisho ulioamua hatma ya ubingwa, Serengeti Girls walitoka sare tasa ya 0-0 dhidi ya wenyeji, Tunisia.

Licha ya matokeo hayo, Serengeti Girls waliendelea kuongoza msimamo wa mashindano kwa alama 7 na tofauti ya mabao ya +5, na hivyo kuwashinda wenyeji Tunisia ambao walikuwa na alama sawa lakini tofauti ya mabao ya +3. Ushindi huu ni ishara ya jitihada kubwa zinazowekwa katika kukuza vipaji vya wasichana wa Tanzania kwenye soka la kimataifa.

Serengeti Girls Waibuka Mabingwa Kombe la UNAF U17 Tunisia 2024

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Jeraha la misuli ya paja Kumuweka Bangala nje kwa zaidi ya wiki moja
  2. Moto Utawaka Msimu wa Ligi ya Championship 2024/2025
  3. Taifa Stars Yasafiri Kuelekea Yamoussoukro Kukabiliana na Guinea
  4. Yanga Kuvaana na CBE Sept 14, Gamondi Aanza Maandalizi Mapema
  5. Kocha Paul Nkata Ajipanga Upya Baada ya Mwanzo Mbaya Ligi Kuu
  6. Simba yaeka Marengo Ya CAF, Mo Dewji Arejea Kuongoza Mikakati
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo