Sandaland Yamtaka Ally Kamwe Kulipa Billion 3 Ndani Ya Siku 7
Kampuni ya Kisheria inayomsimamia Mfanyabiashara Sandaland the Only One ambaye ndie Mtengenezaji wa jezi za SIMBA imemtumia barua Meneja habari na mawasiliano wa Yanga, Ally Kamwe ikidai fidia ya Bilioni Tatu kutokana na kauli za kumchafua mteja wao na kupelekea kuathiri biashara zake. Kamwe anadaiwa kutoa maneno kuwa viongozi wa Simba wamemsema sana Sandaland kuwa wanatukanwa kisa yeye na wakamsusia uzinduzi wa jezi ndio maana akaenda kufanyia dukani kwake.
Kwenye Chapisho hilo wanataka Kamwe afanye mambo yafuatayo:
1- Kulipa fidia ya 3,000,000,000
2- Kumwomba msamaha hadharani Sandaland kwa kumkashfu kuwa anazalisha jezi mbaya hazina ubora.
3- Anapaswa kuomba msamaha kwa Umma kupitia vyombo vya habari vile vile alivyotumia kuongea alichoongea.
4- Ana siku saba (7) za kufanya yote hayo nje na hapo hatua kali zaidi watazichukua.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Camara Aonya Kuhusu Ugumu wa Michuano ya CAF
- Simba na Yanga Zaekwa Kiporo Ratiba Mpya ya Kombe la FA
- Yanga Yapania Kurejea Kwa Kasi ya kimbunga Ligi Kuu
- Luhende Aonya Mastaa wa Soka Kuhusu Starehe Kupita Kiasi
- Mapambano Makali Yanaendelea Championship 2024/2025
- Tanzania Yapanda kwa kasi katika Viwango vya FIFA
Leave a Reply