Rupia Atupia Goli lake la 10 na Kuipa Singida Big Stars Pointi 3 Muhimu Dhidi ya Azam FC

Rupia Atupia Goli lake la 10 na Kuipa Singida Big Stars Pointi 3 Muhimu Dhidi ya Azam FC

Rupia Atupia Goli lake la 10 na Kuipa Singida Big Stars Pointi 3 Muhimu Dhidi ya Azam FC

Wanalambalamba, Azam FC wamekubali kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Singida Big Stars katika uwanja wa CCM Liti mkoani Singida, kufuatia bao pekee la mchezo huo kufungwa na mshambuliaji wa kimataifa kutoka Kenya, Elvis Rupia. Bao hilo lilifungwa dakika ya 75 na kumuwezesha kufikisha mabao 10 kwenye msimu huu wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara.

Ushindi huo ni wa thamani kubwa kwa Singida Big Stars, kwani sasa wamefikisha pointi 50 baada ya mechi 25. Timu hiyo sasa ipo nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi, ikiwa nyuma kwa alama moja tu dhidi ya Azam FC waliopo nafasi ya tatu kwa pointi 51. Matokeo haya yanaonyesha wazi ushindani mkali katika vita ya nafasi nne za juu za msimu huu.

Rupia Atupia Goli lake la 10 na Kuipa Singida Big Stars Pointi 3 Muhimu Dhidi ya Azam FC

Mechi ya Kisasi kwa Singida

Mchezo huu uliokuwa wa kisasi kwa Singida Big Stars, umechezwa kwa ushindani mkubwa kufuatia kumbukumbu ya kupoteza mzunguko wa kwanza dhidi ya Azam FC kwa mabao 2-1. Katika mechi hiyo ya Novemba 28, 2024 kwenye uwanja wa Azam Complex, Elvis Rupia pia alifunga bao la kufutia machozi kwa upande wa Singida.

Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza, Azam walipata mabao yao kupitia kwa Feisal Salum ‘Fei Toto’ dakika ya 38 na Jhonier Blanco dakika ya 56, kabla ya Rupia kujibu kwa bao dakika ya 62.

Takwimu Muhimu za Msimu kwa Singida na Azam

Singida Big Stars sasa wamecheza mechi 25, wakishinda 15, kutoka sare tano na kupoteza tano. Mafanikio haya yanaendelea kuimarisha nafasi yao katika mbio za kumaliza katika nafasi nne za juu za Ligi Kuu.

Aidha, ushindi dhidi ya Azam FC umeendeleza rekodi nzuri ya timu hiyo ambayo haijapoteza katika mechi zake tano zilizopita tangu ilipofungwa na Yanga SC kwa mabao 2-1 Februari 2, 2025 katika uwanja wa KMC Complex.

Kwa upande wa Azam FC, kipigo hiki ni cha nne msimu huu baada ya kushinda mechi 15 na kutoka sare sita.

Timu hiyo sasa ina mtihani mgumu mbele yake katika mchezo unaofuata, ‘Mzizima Derby’ dhidi ya mabingwa watetezi Yanga SC, unaotarajiwa kuchezwa Alhamisi tarehe 10 Aprili 2025.

Rupia Azidi Kung’ara

Kwa upande wa mfungaji wa bao pekee katika mchezo huu, Elvis Rupia ameendelea kuonesha ubora wake msimu huu, na kufikisha mabao 10 kwenye Ligi Kuu Bara. Anafuatia kwa karibu orodha ya wafungaji bora ambapo kinara hadi sasa ni Jean Charles Ahoua wa Simba SC mwenye mabao 12, akifuatiwa na Clement Mzize na Prince wa Yanga wenye mabao 11 kila mmoja.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Man United Walazimishwa Sare na Man City Nyumbani Old Trafford
  2. Prince Dube Afukuzia Rekodi Yake Yanga Kimya Kimya
  3. PSG Yatwaa Ubingwa Ligi Kuu Ufaransa 2024/2025 Huku wakiwa Bado na Michezo 6
  4. Mambo Bado Yamoto Ligi Kuu Tanzania
  5. Yanga Yaingia Mawindondi Kuisaka Saini ya Mohamed Omar Ali
  6. Fei Toto Aelezea Umuhimu wa Mechi Sita Zilizosalia Kwa Azam
  7. De Bruyne Atangaza Kuondoka Man city Mwishoni Mwa Msimu
  8. Ratiba Ya Robo Fainali Crdb Bank Federation Cup 2024/2025
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo