Ratiba ya Taifa Stars Kufuzu AFCON 2025

Ratiba ya Taifa Stars Kufuzu AFCON 2025

Ratiba ya Taifa Stars Kufuzu AFCON 2025

Katika juhudi za kuwania nafasi kwenye fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025, timu ya Taifa Stars ya Tanzania inakabiliwa na changamoto kubwa katika kundi H. Fainali hizi zinatarajiwa kufanyika nchini Morocco kuanzia Desemba 21, 2025, hadi Januari 18, 2026. Taifa Stars imepangwa kukabiliana na wapinzani wenye uzoefu mkubwa, ikiwa ni pamoja na timu za DR Congo, Guinea, na Ethiopia.

Ratiba ya Taifa Stars Kufuzu AFCON 2025

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF), mechi za hatua ya makundi kwa ajili ya kufuzu AFCON 2025 zitafanyika kati ya Septemba 2 na Novemba 19, 2024. Katika kipindi hiki cha takriban siku 78, Taifa Stars itahitaji kuweka juhudi kubwa ili kupata tiketi ya kushiriki fainali hizo.

  1. Raundi ya Kwanza: Taifa Stars vs Ethiopia – Septemba 2, 2024 (Nyumbani)
  2. Raundi ya Pili: Guinea vs Taifa Stars – Septemba 10, 2024 (Ugenini)
  3. Raundi ya Tatu: DR Congo vs Taifa Stars – Oktoba 7, 2024 (Ugenini)
  4. Raundi ya Nne: Taifa Stars vs DR Congo – Oktoba 15, 2024 (Nyumbani)
  5. Raundi ya Tano: Ethiopia vs Taifa Stars – Novemba 16, 2024 (Ugenini)
  6. Raundi ya Sita: Taifa Stars vs Guinea – Novemba 19, 2024 (Nyumbani)

Ratiba ya Taifa Stars Kufuzu AFCON 2025 1

Ratiba ya Taifa Stars Kufuzu AFCON 2025

Changamoto Zinazowakabili Taifa Stars

Kikosi cha Taifa Stars kinapambana na changamoto kubwa kutokana na historia ya ushindani dhidi ya wapinzani wake katika kundi H. DR Congo imekuwa na historia ya kutopatikana kwa urahisi katika mechi za kimataifa, ikishinda mara nyingi dhidi ya Tanzania. Guinea, yenye uzoefu wa kushiriki AFCON mara 11, pia ni tishio kubwa, huku Ethiopia ikiwa na rekodi nzuri dhidi ya Taifa Stars.

Katika mechi za awali, Taifa Stars imepata ushindi mmoja tu dhidi ya DR Congo katika mashindano mbalimbali, huku Guinea ikiibuka kidedea katika mechi zote mbili za kirafiki walizocheza. Ethiopia, kwa upande mwingine, imekuwa na rekodi bora zaidi, ikiibuka na ushindi mara saba kati ya mechi 18 walizokutana na Taifa Stars.

Uzoefu wa Timu Zinazocheza na Taifa Stars

Katika kundi H, DR Congo inaonekana kuwa timu yenye mafanikio zaidi, ikiwa imewahi kutwaa ubingwa wa AFCON mara mbili na kushiriki mara 20. Ikiwa DR Congo itafuzu tena, itakuwa mara yao ya 21 kushiriki AFCON. Guinea inashikilia nafasi ya pili kwa ushiriki mwingi, huku mafanikio yake makubwa yakiwa ni kumaliza katika nafasi ya pili mwaka 1976.

Ethiopia, licha ya kutokuwa na mafanikio makubwa ya hivi karibuni, ina historia ya kushinda AFCON mwaka 1962 na kumaliza katika nafasi ya pili mwaka 1957. Hii inawapa nafasi kubwa ya kuwa wapinzani wenye nguvu dhidi ya Taifa Stars.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Vinara wa Assist NBC Premier League 2024/2025
  2. Wachezaji wa Yanga Walioitwa Timu ya Taifa Stars Agosti 2024
  3. Kikosi cha Taifa Stars Kufuzu AFCON 2025
  4. Ratiba ya yanga Klabu Bingwa CAF 2024/2025
  5. Tabora united Yaibuka na Ushindi wa 2-1 Dhidi ya Namungo
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo