Ratiba ya Mpumalanga Premier international Cup 2024

Ratiba ya Mpumalanga Premier international Cup 2024 | Ratiba ya Yanga Kombe la Mataifa Mpumalanga Cup

Baada ya kumaliza msimu wa 2023/2024 kwa mafanikio makubwa ikiwemo kushinda kombe la ligi kuu Tanzania, kutetea ubingwa wa Kombe la shirikisho na kumaliza katika hatua za robo fainali za CAF Champions league, Klabu ya Yanga inatarajia kuuanza msimu mpya wa 2024/2025 kwa nguvu ileile baada ya kufanya usajili wa wachezaji wengine wenye uwezo mkubwa.

Wakati ligi kuu ya Tanzania ikikaribia kuanza, Klabu ya Yanga imeharikwa kushiriki michuano ya kimataifa ya Mpumalanga Premier International Cup 2024 ambayo inafanyika Afrika Kusini kuanzia tarehe 20 Julai hadi 27 Julai.

Michuano hii inatarajiwa kuwa sehemu muhimu ya maandalizi ya Yanga kuelekea msimu mpya wa ligi kuu Tanzania bara ya NBC, kombe la shirikisho (CRDB Federation Cup) pamoja na michuano ya kimataifa ya klabu bingwa Afrika (CAF Champions league).

Michuano ya Mpumalanga Premier International Cup ni fursa ya pekee kwa klabu mbalimbali kujiweka sawa kimbinu na kimwili kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi. Pia michuano hii inatoa fursa kwa makocha kujaribu mbinu na mifumo mipya ya uchezaji, na kuona ni wachezaji gani watakuwa muhimu zaidi kwenye kikosi chao hasa kwa wachezaji waliosajiliwa katika dirisha hili la usajili.

Ratiba ya Mpumalanga Premier international Cup 2024

Ratiba ya Mpumalanga Premier international Cup 2024

Tarehe 20 Julai 2024

  • FC Augsburg (Ujerumani) dhidi ya Young Africans (Tanzania) saa 3:00 asubuhi kwa saa za Afrika Mashariki
  • TS Galaxy (Afrika Kusini) dhidi ya Mbabane Swallows (Eswatini) saa 8:00 mchana kwa saa za Afrika Mashariki.

Tarehe 27 Julai 2024

  • TS Galaxy (Afrika Kusini) dhidi ya FC Augsburg (Ujerumani) saa 3:00 asubuhi kwa saa za Afrika Mashariki.

Mechi ya Yanga dhidi ya FC Augsburg – Julai 20

Mchezo wa kwanza wa Yanga katika michuano ya Mpumalanga Premier International Cup utakuwa dhidi ya FC Augsburg, klabu inayoshiriki ligi kuu ya Ujerumani maarufu kama Bundesliga. Hii itakuwa mechi ya kihistoria kwa Augsburg ambao watakuwa wakifanya maandalizi yao nje ya Ulaya kwa mara ya kwanza. Mashabiki wa soka haswa wale wa timu ya Yanga Sc wanatarajia kwa hamu kuona jinsi Yanga watakavyoweza kupambana na timu bora kutoka Bundesliga, hasa baada ya usajili wao wa wachezaji wapya wenye uzoefu.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Cv ya Awesu Ali Awesu Kiungo Mpya Simba 2024/2025
  2. Jezi Mpya Za Azam Fc 2024/2025
  3. Jezi Mpya Za Yanga 2024/2025
  4. Ratiba ya Ligi Kuu Tanzania Bara 2024/2025 (NBC Premier league)
  5. Kalenda ya Matukio Msimu wa 2024-2025
  6. Wachezaji Waliosajiliwa Mashujaa Fc 2024/2025
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo