Ratiba ya Mechi za Yanga Ligi Kuu NBC 2024/2025

Ratiba ya Mechi za Yanga Ligi Kuu NBC 2024/2025

Ligi Kuu Tanzania Bara (NBC Premier League) msimu wa 2024/2025 unakaribia kuanza rasmi! na mashabiki wa soka kote nchini wanasubiri kwa hamu kuona timu yao pendwa ikipambana uwanjani.

Mabingwa watetezi Yanga SC, wakiwa na kiu ya kutwaa ubingwa wa nne mfululizo, watakuwa na safari ndefu na yenye changamoto nyingi. Tumekuandalia ratiba kamili ya mechi zao ili uweze kufuatilia kila hatua ya safari hii ya kusisimua.

Yanga wataanza kampeni yao ya ubingwa kwa mchezo mgumu ugenini dhidi ya Kagera Sugar katika Dimba la Kaitaba. Hii itakuwa mechi ya kwanza kati ya mechi 10 za awali ambazo zitatoa taswira ya awali ya uwezo wa Yanga msimu huu. Baada ya hapo, watakabiliana na KenGold FC, timu nyingine inayotarajiwa kutoa upinzani mkali.

Msimu huu, Yanga watatumia Azam Complex kama uwanja wao wa nyumbani kwa sehemu kubwa ya mechi zao. Hii itakuwa fursa nzuri kwa mashabiki wa Yanga walioko Dar es Salaam kuwashuhudia mabingwa wao wakicheza mara kwa mara. Mechi ya kwanza nyumbani itakuwa dhidi ya JKT Tanzania, ikifuatiwa na mchezo dhidi ya Mashujaa FC.

Katikati ya msimu, Yanga watakabiliwa na michezo kadhaa mikubwa, ikiwa ni pamoja na mechi ya ugenini dhidi ya Singida Big Stars na mechi ya nyumbani dhidi ya KMC FC. Lakini, mechi ambayo kila shabiki wa soka Tanzania anasubiri kwa hamu ni “Dabi la Kariakoo” dhidi ya watani wao wa jadi Simba SC. Mechi hii itakuwa kipimo kikubwa kwa Yanga na itaonyesha kama wako tayari kutetea ubingwa wao.

Ratiba ya Mechi za Yanga Ligi Kuu NBC 2024/2025

  1. Kagera Sugar vs Yanga (Ugenini)
  2. KenGold FC vs Yanga (Ugenini)
  3. Yanga vs JKT Tanzania (Nyumbani)
  4. Yanga vs Mashujaa FC (Nyumbani)
  5. Singida BS vs Yanga (Ugenini)
  6. Yanga vs KMC FC (Nyumbani)
  7. Yanga vs Pamba Jiji (Nyumbani)
  8. Simba vs Yanga (Ugenini) – Dabi la Kariakoo
  9. Yanga vs Tabora Utd (Nyumbani)
  10. Coastal Union vs Yanga (Ugenini)

Ratiba ya Mechi za Yanga Ligi Kuu NBC 2024/2025

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Ratiba ya Ligi Kuu Tanzania Bara 2024/2025 (NBC Premier league)
  2. Man City Washinda Ngao ya Jamii 2024 Baada ya Kuichapa Man United Kwa Penalti
  3. Ratiba ya Simba Sc Ligi Kuu Ya NBC 2024/2025
  4. Ratiba ya Fainali Ngao Ya Jamii 2024
  5. Rekodi za Simba na Yanga Kufungana
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo