Ratiba ya Mechi za Simba Machi 2025

Ratiba ya Mechi za Simba Machi 2025

Ratiba ya Mechi za Simba Machi 2025

Wekundu wa Msimbazi, Simba SC, wataingia kwenye mwezi wa Machi 2025 wakiwa na ratiba yenye ushindani mkubwa katika michuano ya Ligi Kuu ya NBC Premier League pamoja na CRDB Federation Cup. Kwa kuwa Yanga SC wanaongoza mbio za kuwania ubingwa wa ligi, Simba SC italazimika kupambana kuhakikisha wanabaki kwenye kinyang’anyiro hicho ili kutetea heshima yao. Ikiwa wewe ni shabiki wa Simba au mpenzi wa soka kwa ujumla, basi hapa tumekuandalia ratiba kamili ya mechi za Simba SC mwezi Machi 2025.

Ratiba Kamili ya Mechi za Simba SC Machi 2025

Ratiba ya Mechi za Simba Machi 2025

1. Coastal Union vs Simba SC

  • 📅 Tarehe: 01 Machi 2025
  • 🏟 Uwanja: Mkwakwani Stadium, Tanga
  • ⚽ Mashindano: Ligi Kuu ya NBC

Simba SC itaanza mwezi wa Machi kwa safari kuelekea Tanga, ambako watakutana na Coastal Union katika Uwanja wa Mkwakwani. Mechi hii inatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa, kwani Coastal Union mara zote wamekuwa wapinzani wenye ushindani wanapocheza nyumbani.

2. Yanga SC vs Simba SC

  • 📅 Tarehe: 08 Machi 2025
  • 🏟 Uwanja: Benjamin Mkapa Stadium, Dar es Salaam
  • ⚽ Mashindano: Ligi Kuu ya NBC

Hii ndiyo mechi inayosubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka nchini—Kariakoo Derby! Simba SC itakutana na mahasimu wao wa jadi, Yanga SC, katika Uwanja wa Benjamin Mkapa. Mchezo huu utakuwa na umuhimu mkubwa katika kuamua hatma ya mbio za ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC msimu huu.

3. Simba SC vs TMA Stars

  • 📅 Tarehe: 11 Machi 2025
  • 🏟 Uwanja: Benjamin Mkapa Stadium, Dar es Salaam
  • ⚽ Mashindano: CRDB Federation Cup

Baada ya kumaliza majukumu yao katika ligi, Simba SC wataelekeza nguvu zao kwenye CRDB Federation Cup kwa mchezo dhidi ya TMA Stars. Mechi hii ni fursa nzuri kwa Simba kuonyesha uwezo wao katika mashindano ya mtoano, huku wakiwa na lengo la kutwaa taji hili muhimu.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Simba Yaivuruga Rekodi ya Mwambusi Arusha
  2. Amrouche Atangazwa Kocha Mpya wa Timu ya Taifa ya Rwanda
  3. Baraka Majogoro Karibu Kujiunga na Orlando Pirates
  4. Hat Trick Dhidi ya Coastal Yampa Mukwala Mzuka Kuelekea Dabi ya Kariakoo
  5. Matokeo ya Coastal Union vs Simba Leo 01/03/2025
  6. Kikosi cha Simba vs Coastal Union Leo 01/03/2025
  7. Coastal Union Vs Simba Leo 01/03/2025 Saa Ngapi?
  8. Mashujaa FC Yathibitisha Kumfuta Kazi Kocha Mohamed Abdallah ‘Baress’
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo