Ratiba ya Mechi za Ligi Kuu ya NBC Leo Septemba 29, 2024

Ratiba ya Mechi za Ligi Kuu ya NBC Leo Septemba 29

Ratiba ya Mechi za Ligi Kuu ya NBC Leo Septemba 29, 2024 | Ratiba ya mechi za leo Ligi Kuu

Leo ni jumapili maalum kwa mashabiki wa soka Tanzania, kwani Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2024/2025 itaendelea kwa michezo minne ya moto itakayopigwa katika viwanja mbalimbali nchini. Kama wewe ni shabiki wa kandanda safu, basi leo ni siku ya kukaa karibu na runinga yako au kwenda viwanjani kushuhudia burudani hii ya kipekee.

Ligi Kuu ya NBC imekuwa ikizidi kuvutia mwaka hadi mwaka, na msimu huu wa 2024/2025 umeonyesha ushindani mkubwa baina ya timu. Hii imeongeza msisimko na kusababisha mashabiki kutarajia matokeo yanayoweza kubadili hali ya msimamo wa ligi. Kwa sasa, Fountain Gate FC inaongoza ligi ikiwa na pointi 13, ikifuatiwa kwa karibu na Singida BS yenye alama 12.

Leo, Septemba 29, 2024, mashabiki wa soka nchini watafurahia michezo minne, ikiwamo ile ya vigogo Simba SC, Yanga SC, Azam FC na timu nyingine zenye upinzani mkali. Mechi hizi zote zitakutanisha timu zinazowania nafasi za juu kwenye msimamo wa ligi.

Ratiba ya Mechi za Ligi Kuu ya NBC Leo Septemba 29, 2024

Ratiba ya Mechi za Ligi Kuu ya NBC Leo Septemba 29, 2024

1. Singida BS vs JKT Tanzania (Saa 8:00 Mchana) – Uwanja wa Liti, Singida

Mchezo wa kwanza utaanza saa 8:00 mchana katika Uwanja wa Liti, Singida, ambapo Singida BS itakuwa wenyeji wa JKT Tanzania. Singida BS inaingia katika mechi hii ikiwa na morali ya ushindi baada ya kuifunga Tabora United kwa mabao 3-1. Kwa upande wa JKT Tanzania, nao walishinda mchezo wao wa mwisho dhidi ya Coastal Union kwa ushindi wa 2-1.

Mchezo huu una umuhimu mkubwa kwa Singida BS kwani ushindi utawafanya kurejea kileleni mwa msimamo wa ligi kwa kufikisha pointi 15. Kwa JKT, ushindi utawapa pointi 9 na kujiweka pazuri kwenye nafasi za kati za msimamo. Hivyo, timu zote mbili zitaingia uwanjani zikiwa na malengo ya kupata pointi muhimu.

2. Mashujaa FC vs Azam FC (Saa 10:00 Alasiri) – Uwanja wa Lake Tanganyika

Baada ya mchezo wa Singida BS, tutashuhudia Mashujaa FC wakiwa wenyeji wa Azam FC katika Uwanja wa Lake Tanganyika. Mashujaa wanaingia uwanjani wakiwa hawajapoteza mechi yoyote msimu huu, wakiwa wameshinda mara mbili na kutoka sare mara mbili.

Azam FC kwa upande wao walipoteza mchezo wao uliopita dhidi ya Simba SC kwa mabao 2-0, na leo watahitaji ushindi ili kurejesha hali ya kujiamini. Mashujaa walitoka sare ya 2-2 dhidi ya Pamba katika mechi yao iliyopita, na hivyo mchezo wa leo ni muhimu kwa timu zote mbili.

3. Dodoma Jiji FC vs Simba SC (Saa 12:30 Jioni) – Uwanja wa Jamhuri, Dodoma

Kuanzia saa 12:30 jioni, mashabiki wa soka wataelekeza macho yao kwenye Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, ambapo Dodoma Jiji FC itawakaribisha Simba SC. Simba SC imeanza msimu vizuri kwa kushinda mechi zote tatu za awali huku wakifunga mabao 9 bila kuruhusu bao hata moja.

Dodoma Jiji, kwa upande wao, hawajapata ushindi katika mechi zao tatu zilizopita, huku wakilazimishwa sare mbili na kushinda mara moja tu msimu huu. Hivyo, mchezo wa leo ni fursa kwao kubadili hali yao na kufuta rekodi mbaya ya kupoteza mechi zote nane dhidi ya Simba SC walizokutana nazo katika historia ya ligi kuu.

4. Yanga SC vs KMC FC (Saa 3:00 Usiku) – Uwanja wa Azam Complex, Chamazi

Mechi ya kufunga siku hii ya michezo itakuwa kati ya Yanga SC na KMC FC, itakayopigwa saa 3:00 usiku katika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi. Yanga SC, mabingwa watetezi wa Ligi Kuu, wanatafuta kuendelea na mwendo wao mzuri baada ya kushinda mechi zao mbili za awali za ligi, huku wakifunga mabao matatu bila kuruhusu bao lolote.

KMC FC, kwa upande wao, wamekuwa na mwanzo mbaya wa msimu huu, wakiwa wameshinda mchezo mmoja tu, kutoka sare mara moja, na kupoteza michezo mitatu. Yanga wanaingia uwanjani wakiwa na kumbukumbu nzuri dhidi ya KMC, kwani wameshinda mechi 9 kati ya 12 walizokutana nazo kwenye ligi.

Mapednekezo ya Mhariri:

  1. Gomez Aanza Mikwara Ligi Kuu Bara, Aahidi Mabao Zaidi
  2. Kocha wa Kagera Sugar Matatani Baada ya Kipigo Kingine
  3. Viwango vya Mzize na Dube Vyampa Kazi Baleke Yanga
  4. FIFA Yaitandika Yanga Faini Nzito Kufuatia Kesi ya Okrah
  5. Mbeya City Yaibuka na Ushindi wa 1-0 Dhidi ya Mbeya Kwanza
  6. Moussa Camara Ajivunia Kamati ya Ulinzi Simba
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo