Ratiba ya Mechi za Leo 19/04/2025 Ligi Kuu NBC
Ligi kuu tanzania bara almaharufu kama ligi kuu ya NBC leo itaendelea kutimua vumbi huku mashabiki wataweza kushuhudia vilabu mbalimbali vikipigania pointi tatu muhimu ili kuendelea kujiimarisha katika mbio za kuusaka ubingwa na wenginge kujiweka mbali zaidi na hatari ya kushuka Daraja. Hapa tumekuletea ratiba kamili ya michezo itakayo pigwa leo April 19 katika viwanja mbalimbali.
1. Singida BS vs Tabora United
Mchezo wa kwanza utawakutanisha wenyeji Singida Big Stars dhidi ya Tabora United katika pambano litakalopigwa majira ya saa 4:00 usiku (saa 10:00 jioni). Hii ni mechi yenye mvuto mkubwa kwa kuwa kila upande unahitaji pointi muhimu kujiimarisha kwenye msimamo wa ligi. Mashabiki wanaweza kufuatilia mchezo huu mubashara kupitia chaneli ya Azam Sports 1 HD.
2. Kagera Sugar vs Azam FC
Baada ya pambano la Singida, macho ya mashabiki yataelekezwa mkoani Kagera ambako wenyeji Kagera Sugar watawakaribisha vigogo wa soka la Tanzania, Azam FC, katika mechi itakayopigwa kuanzia saa 7:00 usiku (saa 1:00 alfajiri). Mchezo huu pia utarushwa moja kwa moja kupitia Azam Sports 1 HD, na unatarajiwa kuwa na ushindani mkali kutokana na uwezo mkubwa wa vikosi vyote viwili.
Kwa kuwa msimu unaelekea ukingoni, kila mchezo una uzito mkubwa katika kuamua hatma ya timu kwenye msimamo wa ligi. Timu kama Azam FC zinalenga kuhakikisha zinapata pointi tatu ili kuendeleza mbio za ubingwa au kutafuta nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa. Kwa upande mwingine, timu kama Tabora United zinahitaji ushindi kujinusuru dhidi ya hatari ya kushuka daraja.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Msigwa Afunguka Kuhusu Ukarabati wa Uwanja wa Mkapa
- Polisi Tanzania Yajipanga Kulpa Kisasi Dhidi ya Mbeya City Babati
- Ifahamu Jayrutty Investment Company Limited, Mdhamini Mpya wa Simba
- Wafungaji Bora CRDB Bank Federation Cup 2024/2025
- Timu Zilizofuzu Nusu Fainali Klabu bingwa UEFA Champions 2024/2025
- Simba SC Yasaini Mkataba Mnono wa Vifaa vya Michezo
- Ratiba ya CRDB Federation Cup Fixtures 2024/2025
- Vilabu Bora Afrika 2024/2025 (CAF Club Ranking)
Leave a Reply