Ratiba ya Mechi za Kufuzu CHAN 2024 Ukanda wa CECAFA

Ratiba ya Mechi za Kufuzu CHAN 2024 Ukanda wa CECAFA

Ratiba ya Mechi za Kufuzu CHAN 2024 Ukanda wa CECAFA

Michuano ya African Nations Championship (CHAN) 2024 inatarajiwa kufanyika mwezi Februari mwaka 2025 katika mataifa matatu ya Afrika Mashariki: Tanzania, Kenya, na Uganda. Mashindano haya yanajulikana kwa kuhusisha wachezaji wanaocheza ligi za ndani ya bara la Afrika pekee, na yanaendelea kuwa jukwaa muhimu kwa wachezaji kuonyesha vipaji vyao. Hata hivyo, kabla ya fainali hizi kufanyika, timu kutoka kanda mbalimba ikiwemo ukanda wa CECAFA zinapitia mchakato wa kufuzu ambao umeanza rasmi kwa mechi za mtoano.

Mfumo wa Kufuzu Ukanda wa CECAFA

Kwa mujibu wa droo iliyofanyika hivi karibuni, nchi kutoka Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) zimepangiwa ratiba ya mechi za kufuzu CHAN 2024. Tanzania, Kenya, na Uganda, ambao ni wenyeji wa michuano hiyo, wamepata nafasi ya moja kwa moja kushiriki fainali. Hata hivyo, timu nyingine kutoka ukanda huu zitaendelea kupambana kufuzu kwa nafasi ya ziada kwa ajili ya kuungana na wenyeji.

Ratiba ya Mechi za Kufuzu CHAN 2024 CECAFA

Mechi za mtoano za kufuzu michuano ya CHAN zitaanza mwezi Oktoba mwaka huu kwa raundi ya kwanza, huku raundi ya pili ikitarajiwa kuchezwa mwezi Desemba 2024. Mashindano haya yamepangwa kwa kuzingatia kanda mbalimbali za Shirikisho la Soka Afrika (CAF), ambapo kila kanda itatoa wawakilishi wake kwenye fainali za CHAN 2024.

Ratiba ya Mechi za Raundi ya Kwanza

Katika droo ya CECAFA, timu kadhaa zimepangiwa kuanza raundi ya kwanza ya mechi za kufuzu:

  • Burundi vs Somalia
  • Ethiopia vs Eritrea
  • Sudan vs Tanzania
  • South Sudan vs Kenya
  • Djibouti vs Rwanda

Tanzania, ambayo itaanza kampeni zake za kufuzu kwa kucheza dhidi ya Sudan, itakuwa na nafasi nzuri endapo itafanikiwa kushinda mchezo huo. Ikiwa itafuzu, Tanzania itakutana na mshindi kati ya Ethiopia na Eritrea kwenye raundi ya pili.

Uganda, moja ya wenyeji wa michuano, itajiunga na raundi ya pili moja kwa moja na itakutana na mshindi wa mechi kati ya Burundi na Somalia.

Ratiba ya Raundi ya Pili

Timu zitakazoshinda mechi za raundi ya kwanza zitasonga mbele na kucheza raundi ya pili mwezi Desemba mwaka huu, na ratiba inaonyesha mechi zifuatazo:

  • Burundi/Somalia vs Uganda
  • Ethiopia/Eritrea vs Sudan/Tanzania
  • South Sudan/Kenya vs Djibouti/Rwanda

Ratiba ya Mechi za Kufuzu CHAN 2024 Ukanda wa CECAFA

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Ratiba Ligi Kuu ya Wanawake (TWPL) 2024/2025
  2. Chama- Ndoto ya Ubingwa wa Afrika na Yanga Inawezekana!
  3. Kikao Cha Masaa Saba Man Utd Chamalizika Bila Taarifa ya Hatma ya Ten Hag
  4. Timu 5 Zinazopewa Nafasi Kubwa Kushindwa Klabu Bingwa Ulaya 2024/2025
  5. Andres Iniesta Atundika Daluga Baada ya Miaka 22 Ndani ya Soka la Kulipwa
  6. Taifa Stars Kusaka Ushindi Dhidi ya DRC Congo Oktoba 10
  7. Coastal Union na Yanga Zakumbana na Rungu la TPLB Kisa Uchelewaji
  8. Simba na Yanga Kukabiliana na Vigogo Michuano ya CAF Afrika
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo