Ratiba ya Ligi Kuu Tanzania Bara 2024/2025 (NBC Premier league)

Ratiba ya Ligi Kuu Tanzania Bara 2024/2025 (Ratiba ya NBC Premier league 2024/2025): Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2024-2025, maarufu kama NBC Premier League 2024/2025, inatarajiwa kuanza kwa kishindo mnamo tarehe 16 Agosti 2024. Msimu huu unatarajiwa kua msimu wa kusisimua zaidi, ukiwa na timu 16 zitakazoshindana vikali kuwania taji la ubingwa.

Ratiba ya Ligi Kuu Tanzania Bara (Ratiba ya NBC Premier league 2024/2025)

Ratiba ya Ligi Kuu Tanzania Bara (Ratiba ya NBC Premier league 2024/2025)

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL) imetangaza rasmi kuanza kwa msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2024-25, utakaoanza mnamo Agosti 16, 2024. Msimu huu unatarajiwa wenye ushindani mkubwa kutokana na maboresho yaliofanyika katika vikosi vya timu mbalimbali ambazo zote zimeonesha wazi nia ya kuwapa Yanga Sc changamoto ya kutetea ubingwa wao.

Kabla ya kuanza kwa ligi kuu, mashabiki wa soka watashuhudia mchezo wa Ngao ya Jamii, ambayo utachezwa kati ya Agosti 8 na 11, 2024. Mechi hii ya jadi itakuwa ni kipimo cha awali cha uwezo wa timu kabla ya kuanza kwa msimu rasmi.

Msimu wa 2024/2024 wa ligi kuu utakuwa na mizunguko 30, ambapo kila timu itacheza dhidi ya nyingine mara mbili, nyumbani na ugenini. Msimu unatarajiwa kumalizika tarehe 24 Mei 2025, na kutakuwa na dirisha dogo la usajili litakalofunguliwa tarehe 15 Desemba 2024 hadi 15 Januari 2025, ambapo timu zitakuwa na fursa ya kuimarisha vikosi vyao.

Yanga SC, mabingwa watetezi wa msimu uliopita wa 2023-24, watakuwa na kibarua cha kutetea taji lao dhidi ya timu nyingine zenye nguvu. Msimu huu, ligi kuu itawakaribisha wageni wapya, Kengold FC kutoka Tukuyu, Mbeya, na Pamba Jiji FC kutoka Mwanza, ambao wamepanda daraja kutoka Ligi Daraja la Kwanza.

Wakati huohuo, Mechi za Ligi Daraja la Kwanza (Championship) zitaanza tarehe 14 Septemba 2024 na kumalizika tarehe 10 Mei 2025.

Fainali ya Kombe la FA, ambayo ni moja ya michuano mikubwa nchini, imepangwa kufanyika tarehe 31 Mei 2025. Msimu huu wa soka nchini Tanzania unaahidi kuwa wa kusisimua na wenye ushindani mkubwa katika ligi zote mbili, huku timu zikipambana vikali kufikia malengo yao. Mashabiki wa soka wanaweza kutarajia burudani ya hali ya juu na vituko vingi katika msimu huu wa 2024-25.

Hii apa Ratiba ya Ligi Kuu Tanzania Bara 2024/2025 (Ratiba ya NBC Premier league 2024/2025)

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) leo imetoa ratiba ya NBC Premier League msimu wa 204/25 ambayo inaonesha itaanza kutimua vumbi Agosti 16, 2024 kwa kuishuhudia mechi moja kati ya Pamba Jiji dhidi ya Tanzania Prisons.

Kwa mujibu wa ratiba hiyo, watani wa jadi watavaana Oktoba 19, 2024 ambapo Simba SC itakuwa mwenyeji dhidi ya Yanga SC. Ratiba hiyo inaonesha kuwa pazia la NBC Premier League litafungwa mnamo Mei 24, 2025 kwa kushuhudia mechi nane majira ya saa 10:00 jioni.

Ratiba ya Ligi Kuu Tanzania Bara 2024/2025 NBC

Ratiba ya Ligi Kuu Tanzania Bara 2024/2025 NBC Premier league

FUATILIA HAPA

  1. Vinara wa Assist NBC Premier League 2024/2025
  2. Wafungaji Bora Ligi Kuu ya NBC Tanzania 2024/2025
  3. Msimamo Ligi Kuu NBC 2024/2025 Tanzania Premier League
  • Mzunguko wa 1: Kuanza Agosti 16, 2024
  • Mzunguko wa 2: Kuanza Agosti 24, 2024
  • Mzunguko wa 3: Kuanza Septemba 11, 2024
  • Mzunguko wa 4: Kuanza Septemba 14, 2024
  • Mzunguko wa 5: Kuanza Septemba 21, 2024
  • Mzunguko wa 6: Kuanza Septemba 28, 2024
  • Mzunguko wa 7: Kuanza Oktoba 2, 2024
  • Mzunguko wa 8: Kuanza Oktoba 19, 2024
  • Mzunguko wa 9: Kuanza Oktoba 26, 2024
  • Mzunguko wa 10: Kuanza Novemba 2, 2024
  • Mzunguko wa 11: Kuanza Novemba 9, 2024
  • Mzunguko wa 12: Kuanza Novemba 23, 2024
  • Mzunguko wa 13: Kuanza Novemba 30, 2024
  • Mzunguko wa 14: Kuanza Desemba 11, 2024
  • Mzunguko wa 15: Kuanza Desemba 14, 2024
  • Mzunguko wa 16: Kuanza Desemba 21, 2024
  • Mzunguko wa 17: Kuanza Desemba 28, 2024
  • Mzunguko wa 18: Kuanza Januari 18, 2025
  • Mzunguko wa 19: Kuanza Januari 25, 2025
  • Mzunguko wa 20: Kuanza Februari Mosi, 2025
  • Mzunguko wa 21: Kuanza Februari 15, 2025
  • Mzunguko wa 22: Kuanza Februari 22, 2025
  • Mzunguko wa 23: Kuanza Machi Mosi, 2025
  • Mzunguko wa 24: Kuanza Machi 8, 2025
  • Mzunguko wa 25: Kuanza Machi 29, 2025
  • Mzunguko wa 26: Kuanza Aprili 12, 2025
  • Mzunguko wa 27: Kuanza Aprili 19, 2025
  • Mzunguko wa 28: Kuanza Mei 3, 2025
  • Mzunguko wa 29: Kuanza Mei 17, 2025
  • Mzunguko wa 30: Kuanza Mei 24, 2025

Tafadhali kumbuka: Ratiba hii inaweza kubadilika kulingana na maamuzi ya TPL na matukio mengine yasiyotarajiwa. Endelea kufuatilia tovuti rasmi ya TPL na vyombo vya habari kwa taarifa zaidi na ratiba iliyosasishwa.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Kalenda ya Matukio Msimu wa 2024-2025
  2. Jezi mpya ya Chelsea Msimu wa 2024/25 Hii hapa
  3. Wachezaji Waliosajiliwa Mashujaa Fc 2024/2025
  4. Mashujaa Fc Imetangaza Kumsajili Carlos Protus
  5. Seleman Mwalimu ‘Gomez’ Asajiliwa Fountain Gate
  6. TETESI ZA USAJILI: Dodoma Jiji FC Katika Mazungumzo ya Kumrejesha Wazir Jr
  7. Khalid Aucho, Kennedy Musonda na Djigui Diarra Warejea Mazoezini
  8. Chama Kuvaa Jezi Namba 17 Yanga Msimu Ujao
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo