Ratiba ya Ligi Kuu Tanzania Bara 2024/2025

Ratiba ya Ligi Kuu Tanzania Bara

Ratiba ya Ligi Kuu Tanzania Bara 2024/2025 | Ratiba ya NBC Premier league 2024/25

Ligi Kuu Tanzania Bara, maarufu kama NBC Premier League, inajiandaa kurejea kwa kishindo mnamo tarehe 16 Agosti 2024. Msimu huu wa 2024/2025 unatarajiwa kuwa wa kipekee, ukiwa na timu 16 zitakazopambana vikali kuwania taji la ubingwa. Maboresho makubwa katika vikosi vya timu mbalimbali yamefanyika, na kila timu inaonesha dhamira ya kuitoa Yanga SC kwenye kiti cha ubingwa.

Muhtasari wa Msimu wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2024/2025

  • Tarehe ya Kuanza: 16 Agosti 2024
  • Tarehe ya Kumalizika: 24 Mei 2025
  • Idadi ya Timu: 16
  • Mizunguko: 30
  • Mabingwa Watetezi: Yanga SC
  • Timu Zilizopanda Daraja: Kengold FC (Tukuyu, Mbeya) na Pamba Jiji FC (Mwanza)
  • Dirisha Dogo la Usajili: 15 Desemba 2024 – 15 Januari 2025

Ratiba ya Ligi Kuu Tanzania Bara 2024/2025

Ratiba ya Ligi Kuu Tanzania Bara 2024/2025

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), kupitia Mtendaji Mkuu wake Almas Kasongo, imethibitisha kuwa ratiba kamili ya msimu itatangazwa ndani ya siku chache zijazo. Hata hivyo, tayari tunajua kuwa msimu utaanza rasmi tarehe 16 Agosti 2024, huku mechi ya Ngao ya Jamii ikipamba ufunguzi wa msimu kati ya tarehe 8 na 11 Agosti 2024. Msimu huu utakuwa na jumla ya mizunguko 30, ambapo kila timu itacheza mara mbili dhidi ya kila mpinzani, nyumbani na ugenini. Kilele cha msimu kinatarajiwa kufikia tarehe 24 Mei 2025.

Ratiba ya Mizunguko Ligi Kuu Tanzania Bara

Ratiba kamili ya mzunguko wa ligi kuu ya Tanzania Bara ni kama ifuatavyo:

  • Mzunguko wa 1: Agosti 16, 2024
  • Mzunguko wa 2: Agosti 24, 2024
  • Mzunguko wa 3: Septemba 11, 2024
  • Mzunguko wa 4: Septemba 14, 2024
  • Mzunguko wa 5: Septemba 21, 2024
  • Mzunguko wa 6: Septemba 28, 2024
  • Mzunguko wa 7: Oktoba 2, 2024
  • Mzunguko wa 8: Oktoba 19, 2024
  • Mzunguko wa 9: Oktoba 26, 2024
  • Mzunguko wa 10: Novemba 2, 2024
  • Mzunguko wa 11: Novemba 9, 2024
  • Mzunguko wa 12: Novemba 23, 2024
  • Mzunguko wa 13: Novemba 30, 2024
  • Mzunguko wa 14: Desemba 11, 2024
  • Mzunguko wa 15: Desemba 14, 2024
  • Mzunguko wa 16: Desemba 21, 2024
  • Mzunguko wa 17: Desemba 28, 2024
  • Mzunguko wa 18: Januari 18, 2025
  • Mzunguko wa 19: Januari 25, 2025
  • Mzunguko wa 20: Februari 1, 2025
  • Mzunguko wa 21: Februari 15, 2025
  • Mzunguko wa 22: Februari 22, 2025
  • Mzunguko wa 23: Machi 1, 2025
  • Mzunguko wa 24: Machi 8, 2025
  • Mzunguko wa 25: Machi 29, 2025
  • Mzunguko wa 26: Aprili 12, 2025
  • Mzunguko wa 27: Aprili 19, 2025
  • Mzunguko wa 28: Mei 3, 2025
  • Mzunguko wa 29: Mei 17, 2025
  • Mzunguko wa 30: Mei 24, 2025

Msimu huu utaendelea kwa mizunguko 30, ambapo kila timu itacheza dhidi ya nyingine mara mbili, nyumbani na ugenini. Ratiba hii inaonesha mapema tarehe na mizunguko ya mechi, lakini inaweza kubadilika kulingana na maamuzi ya TPLB na hali za dharura.

Matukio Muhimu ya Msimu

  • Msimu wa 2024/2025 utajumuisha vipande viwili muhimu kabla ya kuanza kwa ligi kuu:
  • Ngao ya Jamii: Mechi ya awali itakayochukua nafasi kati ya Agosti 8 hadi 11, 2024. Hii ni fursa kwa timu kuonyesha maandalizi yao kabla ya michuano rasmi.
  • Dirisha Dogoo la Usajili: Dirisha hili litafunguliwa tarehe 15 Desemba 2024 na kufungwa tarehe 15 Januari 2025. Timu zitakuwa na nafasi ya kuimarisha vikosi vyao kabla ya hatua muhimu za msimu.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Mshindi wa MVP Ligi Kuu Tanzania Bara NBC 2023/2024 Amepatikana
  2. Orodha ya Makocha Timu za Ligi Kuu ya NBC 2024/2025
  3. Opah Clement Ajiunga Na Henan Fc Ya Ligi Kuu Ya China
  4. Tuzo ya Mchezaji Bora Ligi Kuu NBC 2023/2024: Hawa Ndio Wagombea
  5. Msimamo wa Ligi Kuu ya U17 Tanzania 2024
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo