Ratiba ya Kombe la Shirikisho la CRDB Federation Cup Leo 03/03/2025
KIVUMBI cha michuano ya Kombe la Shirikisho la CRDB Federation Cup kinaendelea leo kwa mechi sita muhimu, ambapo timu 12 kutoka ligi tofauti zitapambana kusaka nafasi ya kufuzu hatua ya 16 Bora. Mchuano huu unazidi kushika kasi huku kila timu ikihitaji ushindi ili kuendelea na safari ya kutwaa taji linalotoa tiketi ya kushiriki Kombe la Shirikisho Afrika.
Katika hatua hii, timu mbili kutoka Ligi Kuu Tanzania Bara, JKT Tanzania na Tabora United, ndizo pekee zitakazoshuka dimbani leo kutafuta tiketi ya kusonga mbele. Tabora United, ambayo imehamishia mchezo wake kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma, itamenyana na Transit Camp, klabu inayoshiriki Ligi ya Championship.
Mechi hii inatarajiwa kuwa na upinzani mkali huku Tabora United ikipambana kufuta machungu ya kushindwa kutumia uwanja wao wa nyumbani, Ali Hassan Mwinyi, ambao umesimamishwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa kutokidhi vigezo vilivyowekwa.
Kwa upande mwingine, JKT Tanzania watakuwa wenyeji wa Biashara United katika Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Dar es Salaam. Biashara United, ambayo kwa sasa inakabiliwa na changamoto kwenye Ligi ya Championship, itakuwa na kibarua kigumu dhidi ya JKT Tanzania ambao wanataka kutumia uzoefu wao wa Ligi Kuu kupata ushindi.
Ratiba Kamili ya Mechi za Leo CRDB Federation Cup (03/03/2025)
- Mbeya Kwanza vs Mambali Ushirikiano – Saa 10:00 jioni
- Polisi Tanzania vs Songea United – Saa 10:00 jioni
- Mtibwa Sugar vs Towns Stars – Saa 10:00 jioni
- Girrafe Academy vs Green Warriors – Saa 10:00 jioni
- JKT Tanzania vs Biashara United – Saa 10:00 jioni
- Tabora United vs Transit Camp – Saa 10:00 jioni
Timu Kubwa Kuingia Dimba Wiki Ijayo
Baada ya mechi hizi za hatua ya 32 Bora, macho yataelekezwa kwa vigogo wa soka nchini, Simba SC na Yanga SC, ambao watashuka dimbani wiki ijayo baada ya kumaliza Dabi ya Kariakoo itakayochezwa Machi 8 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.
Simba SC watafungua dimba Machi 11 kwa kuwakaribisha TMA Stars ya Arusha.
Yanga SC watacheza siku inayofuata Machi 12 dhidi ya Coastal Union, timu waliokutana kwenye fainali ya 2022 na kutoa burudani ya mabao 3-3 kabla ya Yanga kushinda kwa penalti 4-1 na kutwaa ubingwa.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Ratiba ya Mechi za Simba Machi 2025
- Mbeya City Yaing’oa Azam CRDB Bank Federation Cup kwa Mikwaju ya Penati
- Simba Yaivuruga Rekodi ya Mwambusi Arusha
- Amrouche Atangazwa Kocha Mpya wa Timu ya Taifa ya Rwanda
- Baraka Majogoro Karibu Kujiunga na Orlando Pirates
- Hat Trick Dhidi ya Coastal Yampa Mukwala Mzuka Kuelekea Dabi ya Kariakoo
- Matokeo ya Coastal Union vs Simba Leo 01/03/2025
Leave a Reply