Ratiba ya Kombe la Muungano 2025
PAZIA la michuano ya Kombe la Muungano linafunguliwa rasmi Alhamisi, tarehe 24 Aprili 2025, kwa mchezo wa kusisimua wa robo fainali kati ya Singida Black Stars na JKU SC, utakaopigwa saa 11:00 jioni kwenye Uwanja wa Gombani, kisiwani Pemba. Singida inajiunga kwenye mashindano haya kwa mara ya kipekee baada ya Simba SC kujitoa kutokana na ratiba ngumu ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Kwa mwaka huu, Kombe la Muungano linazishirikisha jumla ya timu nane — nne kutoka Tanzania Bara (Azam FC, Coastal Union, Singida Black Stars, na Yanga SC) na nne kutoka Zanzibar (JKU SC, KMKM, KVZ SC na Zimamoto SC). Timu zote zinakabiliana na ndoto moja — kuchukua ubingwa wa mashindano haya yenye historia ndefu tangu yalipoanzishwa mwaka 1982.
Ratiba Robo Fainali Ratiba ya Kombe la Muungano 2025: Vita Ya Kwanza Ya Ubingwa
Mashindano yanaanza kwa robo fainali nne kama ifuatavyo:
JKU SC vs Singida BS SC
- Tarehe: 24 Aprili 2025
- Saa: 11:00 jioni
- Uwanja: Gombani Stadium, Pemba
Zimamoto SC vs Coastal Union SC
- Tarehe: 25 Aprili 2025
- Saa: 10:00 jioni
- Uwanja: Gombani Stadium
KMKM SC vs Azam FC
- Tarehe: 25 Aprili 2025
- Saa: 01:15 usiku
- Uwanja: Gombani Stadium
KVZ FC vs Young Africans SC
- Tarehe: 26 Aprili 2025
- Saa: 01:15 usiku
- Uwanja: Gombani Stadium
Katika mahojiano na vyombo vya habari, Kaimu Kocha Mkuu wa Singida Black Stars, David Ouma, alieleza kuwa mashindano haya ni fursa ya kipekee kwa kikosi chake kuonyesha ubora wao kitaifa, huku wakilenga kutwaa ubingwa.
Kwa mujibu wa Ouma, timu hiyo haijaja Zanzibar kushiriki tu, bali kushindana kikamilifu kwa lengo la kutwaa kombe hilo.
Hata hivyo, Singida itawakosa baadhi ya wachezaji wake tegemeo akiwemo mshambuliaji kinara Jonathan Sowah (Ghana), pamoja na Marouf Tchakei na Ibrahim Imoro. Hii ni kwa mujibu wa taarifa ya Ofisa Habari wa klabu hiyo, Hussein Massanza, ambaye alisisitiza kuwa kikosi kilichosafiri kina uwezo na ari ya kushindana.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Yanga Yaishushia Fountain Gate Kichapo Cha 4-0 na Kuweka Rekodi
- Kikosi cha Yanga VS Fountain Gate Leo 21/04/2025
- Matokeo ya Fountain Gate vs Yanga Leo 21/04/2025
- Fountain Gate FC vs Yanga Leo 21/04/2025 Saa Ngapi?
- Kikosi cha Simba VS Stellenbosch Leo 20/04/2025
- Matokeo ya Simba VS Stellenbosch Leo 20/04/2025
- Simba VS Stellenbosch Leo 20/04/2025 Saa Ngapi?
- Ifahamu Jayrutty Investment Company Limited, Mdhamini Mpya wa Simba
Leave a Reply