Ratiba ya Kombe la Mapinduzi 2025 | Ratiba ya Mapinduzi Cup 2025
Rasmi Kamati ya Maandalizi ya Kombe la Mapinduzi kwa kushirikiana na Shirikisho la Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFF) imetoa ratiba rasmi ya michuano ya Kombe la Mapinduzi kwa mwaka 2025, inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi kuanzia Januari 3 hadi Januari 13, 2025, katika Uwanja wa Gombani, kisiwani Pemba. Mashindano haya ya kihistoria yanaleta ladha tofauti msimu huu kwa kushirikisha timu za taifa za wakubwa, badala ya klabu kama ilivyozoeleka, huku yakitarajiwa kuvutia mashabiki wengi kutoka ndani na nje ya Tanzania.
Kwa mujibu wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFF), Dkt. Suleiman Mahmoud Jabir, ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mapinduzi Cup 2025, mashindano ya msimu huu yatahusisha timu zifuatazo:
- Zanzibar Hero’s (Wenyeji)
- Kilimanjaro Stars (Tanzania Bara)
- Burundi
- Uganda
- Kenya
- Burkina Faso
Mashindano haya ni fursa adhimu kwa timu hizi kuonyesha uwezo wao, huku mshindi wa kwanza akiondoka na zawadi nono ya shilingi milioni 100.
Ratiba ya Kombe la Mapinduzi 2025 | Ratiba ya Mapinduzi Cup 2025
Michuano itaanza rasmi Januari 3, 2025, na kufuatia mechi mbalimbali kulingana na ratiba ifuatayo:
Ijumaa, Januari 3, 2025
- Zanzibar vs Burundi – Saa 2:15 Usiku
Jumamosi, Januari 4, 2025
- Tanzania Bara vs Burkina Faso – Saa 2:15 Usiku
Jumapili, Januari 5, 2025
- Kenya vs Burundi – Saa 2:15 Usiku
Jumatatu, Januari 6, 2025
- Burkina Faso vs Uganda – Saa 2:15 Usiku
Jumanne, Januari 7, 2025
- Zanzibar vs Kenya – Saa 2:15 Usiku
Jumatano, Januari 8, 2025
- Uganda vs Tanzania Bara – Saa 2:15 Usiku
Mapendekezo ya Mhariri:
Leave a Reply