Ratiba ya CRDB Federation Cup Fixtures 2024/2025 | Ratiba ya Robo Fainali Kombe la Shirikisho la CRDB
Kombe la Shirikisho la CRDB Tanzania, linalojulikana pia kama Kombe la FA Tanzania, limefikia hatua muhimu ya msimu wa 2024/2025. Hivi sasa mashindano haya yako katika hatua ya robo fainali, ambapo timu nane zimeingia vitani kuwania tiketi ya kucheza nusu fainali na hatimaye kutinga fainali ya kuwania ubingwa wa kombe hili lenye hadhi ya kipekee katika soka la ndani.
Mashindano haya ambayo hutoa nafasi kwa timu kutoka ligi mbalimbali nchini Tanzania, yameendelea kuonyesha ushindani mkubwa, huku timu kubwa zikipambana na zile zinazokuja kwa kasi katika tasnia ya soka. Hapa Tunaangazia kwa kina ratiba ya mechi zote zilizopangwa kwa robo fainali pamoja na upangaji wa michezo ya nusu fainali kulingana na matokeo ya awamu hii ya mtoano.
🏆 Ratiba ya CRDB Federation Cup Fixtures 2024/2025 Robo Fainali
Robo fainali ya michuano hii imepangwa kuchezwa kati ya tarehe 13 hadi 15 Aprili 2025 katika viwanja mbalimbali nchini, ambapo mechi zote zinatarajiwa kuwa na ushindani mkali. Hii hapa ni ratiba kamili:
13 Aprili 2025:
🔹 Simba SC vs Mbeya City – KMC Stadium
14 Aprili 2025:
🔹 JKT Tanzania vs Pamba Jiji – Uwanja wa Meja Isamuyo
🔹 Singida Big Stars vs Kagera Sugar – Liti Stadium
15 Aprili 2025:
🔹 Young Africans vs Stand United – KMC Stadium
Katika hatua hii, timu zote zinatambua umuhimu wa mechi hizi kwa kuwa ni mtoano wa moja kwa moja, na kila kosa linaweza kugharimu nafasi ya kutinga nusu fainali.
⚽ Mechi za Nusu Fainali – CRDB Federation Cup 2024/25
Baada ya kumalizika kwa michezo ya robo fainali, mechi za nusu fainali zitapangwa kulingana na washindi wa kila pambano kama ifuatavyo:
- Young Africans / Stand United 🆚 JKT Tanzania / Pamba Jiji
- Simba SC / Mbeya City 🆚 Singida BS / Kagera Sugar
Mechi hizi za nusu fainali zinatarajiwa kuchezwa kwa ushindani wa juu, hasa ikizingatiwa kuwa timu kama Simba SC, Yanga SC, na Singida BS zimeonyesha kiwango cha juu msimu huu. Hii ni hatua ya mwisho kabla ya fainali ya CRDB Federation Cup, hivyo mashabiki wa soka wanatarajia burudani ya kiwango cha juu.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Al Ahly Yashindwa Kutamba Mbele ya Pyramids Pungufu
- Mpanzu na Kibu Wamtia Hofu Kocha wa Stellenbosch
- Ratiba ya Simba Nusu Fainali Kombe la Shirikisho Afrika
- Kikosi cha Yanga vs Azam Leo 10/04/2025
- Azam vs Yanga Leo 10/04/2025 Saa Ngapi
- Mikwaju ya Penati Yaipeleka Simba Nusu Fainali Kombe la Shirikisho CAF
- Vituo Vya Kununua Tiketi za Mechi ya Simba VS Al Masry 09/04/2025
Leave a Reply