Rasmi: Simba SC Yamtema Sadio Kanoute
Klabu ya Simba SC inaendelea na zoezi la kuboresha kikosi chake ambapo hadi sasa wamehsatangaza nyota wapya 12 ambao watajiunga na kikosi cha wekundu wa Msimbazi. Mbali na kusajili wachezaji wapya, klabu ya Simba imeendelea kuwaaga wachezaji ambao hawakukidhi malengo ya klabu na wale walioomba kuachana na timu. Leo, Julai 9, Simba SC imetangaza rasmi kuachana na kiungo mkabaji Sadio Kanoute, ambaye ameihudumia klabu hiyo kwa misimu miwili. Taarifa hii imewashangaza wengi, hasa ikizingatiwa mchango mkubwa wa Kanoute katika mafanikio ya hivi karibuni ya Simba SC.
Rasmi: Simba SC Yamtema Sadio Kanoute
Kanoute, aliyejiunga na Simba mwaka 2021 kutoka klabu ya Libya ya Al-Ahli Benghazi, amekuwa nguzo muhimu katika safu ya kiungo ya Wekundu wa Msimbazi. Uwezo wake wa kuchezesha timu, kutoa pasi za mwisho zenye macho, na kufunga mabao muhimu umemfanya kuwa kipenzi cha mashabiki. Uamuzi wa Simba SC kuachana na Kanoute unaashiria mabadiliko makubwa yanayofanyika ndani ya kikosi kuelekea msimu wa 2024/2025. Klabu inalenga kujenga upya kikosi chao ili kuimarisha ushindani wao katika ligi ya ndani na michuano ya kimataifa.
Kuachana na Sadio Kanoute ni sehemu ya mkakati mpana wa Simba SC wa kuimarisha kikosi chao kuelekea msimu ujao. Klabu inaendelea kufanya maboresho katika kila idara ili kuhakikisha wanapata kikosi bora kitakachoweza kushindana na kushinda mataji zaidi. Uongozi wa Simba SC una imani kuwa mabadiliko haya yatasaidia kuongeza ufanisi na ushindani wa timu katika mashindano mbalimbali.
Katika taarifa yao rasmi, Simba SC imetoa shukrani za dhati kwa Sadio Kanoute kwa mchango wake mkubwa katika klabu. Wamemtakia kila la heri katika maisha yake ya soka nje ya Msimbazi.
Mapendekezo ya Mhariri:
Leave a Reply