Picha za Wachezaji Wapya wa Simba 2024/2025
Klabu ya Simba SC, moja ya klabu kongwe na zenye mafanikio makubwa nchini Tanzania, inajiandaa kwa msimu mpya wa 2024/2025 kwa kusajili wachezaji wapya. Msimu uliopita haukuwa mzuri kwa Simba kwani walishindwa kushinda kombe lolote kubwa na walimaliza ligi kuu ya Tanzania katika nafasi ya tatu, kitu ambacho kiliwazuia kupata tiketi ya kushiriki michuano ya Klabu Bingwa Afrika (CAF Champions League). Ili kurejea kwenye ubora wao na kuleta ushindani mkubwa msimu huu, Simba SC imejikita kwenye kusajili wachezaji wenye vipaji na uzoefu mkubwa. Katika makala hii, tutaangazia picha na maelezo ya wachezaji wapya wa Simba kwa msimu wa 2024/2025.
Hawa Ndio Wachezaji Wapya wa Simba 2024/2025
- Lameck Lawi
- Ahoua Jean Charles
- Steven Mukwala
- Joshua Mutale
- Abdulrazak Hamza
Picha za Wachezaji Wapya wa Simba 2024/2025
Simba SC imejitahidi kuimarisha kikosi chake kwa msimu ujao kwa kuwasajili wachezaji ambao wameonesha kiwango cha hali ya juu katika vilabu walivyo kua wanachezea msimu wa 2023/2024. Miongoni mwa usajili muhimu ni pamoja na:
Lameck Lawi
Lawi, mwenye umri wa miaka 18, amesajiliwa kutoka Coastal Union ya Tanga. Anacheza kama beki wa kati na ana uwezo mkubwa wa kuzuia mashambulizi ya adui na kusaidia katika kuanzisha mashambulizi.
Ahoua Jean Charles
Kiungo mshambuliaji kutoka Ivory Coast, Ahoua Jean Charles, amesajiliwa kutoka Stella Club d’Adjamé. Ametambulika kwa uwezo wake wa kufunga mabao na kusaidia wenzake kwa kupitia huo.
Steven Mukwala
Mukwala, mshambuliaji kutoka Asante Kotoko ya Ghana, amesajiliwa kuimarisha safu ya ushambuliaji ya Simba SC. Anatarajiwa kuwa nguzo muhimu katika kufunga magoli.
Joshua Mutale
Mutale, mwenye umri wa miaka 22, anaweza kucheza nafasi mbalimbali uwanjani ikiwemo winga ya kulia na kushoto. Amesajiliwa kutoka Power Dynamos ya Zambia.
Abdulrazak Hamza
Hamza, beki kisiki mrithi wa Henock Inonga baka kutoka SuperSport United ya Afrika Kusini, amejiunga na Simba SC kwa lengo la kuimarisha safu ya ulinzi. Ana uzoefu mkubwa kutokana na kucheza katika ligi tofauti za ndani na nje ya Tanzania.
Debora Fernandes
Augustine Okejepha
Valentino Mashaka
Omary Abdallah Omary
Valentin Nouma
Karaboue Chamou
Yusuph Kagoma
Mapendekezo ya Mhariri:
Leave a Reply