Penati ya Dakika za Majeruhi Yaipa Simba Pointi Tatu Dhidi ya JKT
Wekundu wa Msimbazi Simba leo wamejizoea pointi tatu nyengine japo kwa mbinde dhidi ya maafande wa JKT Tanzania katika mtanange wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa jioni ya leo. Kwa ushindi huo wa bao moja kwa sifuri, Simba imeendelea kuthibitisha nia yao ya kutawala kilele cha msimamo wa ligi kuu ya Tanzania bara.
Mchezo huu ulianza kwa kasi huku kila upande ukijaribu kutawala mchezo. Timu zote zilionyesha ukakamavu mkubwa, lakini hadi mapumziko, hakukuwa na bao lolote lililofungwa. Ulinzi imara wa JKT uliwafanya Simba kujikuta wakihitaji mbinu zaidi kuvunja safu hiyo.
Wakati mashabiki wakiwa tayari wameshakubaliana na sare, penalti ya dakika za majeruhi iligeuza upepo wa mchezo. Jean Charles Ahoua, mshambuliaji wa Simba, alisimama kwa ujasiri kwenye nafasi ya penalti dakika ya 90+4 na kupachika bao safi lililoamua hatima ya mchezo. Hili linakuwa bao lake la saba msimu huu, na kuendelea kuonyesha umuhimu wake ndani ya kikosi cha Simba.
Kwa ushindi huu, Simba sasa imefikisha pointi 37 baada ya kucheza mechi 14, ikiwazidi mahasimu wao wa jadi Young Africans kwa tofauti ya pointi nne. Ushindi huu unaipa Simba nafasi ya kujiimarisha zaidi kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, huku ikijiongezea motisha ya kuendelea kupambana.
Mapendekezo ya Mhariri:
Leave a Reply