Orodha ya Vinara wa Clean Sheets Ulaya
Kuwa na “clean sheet” nyingi ni mojawapo ya mafanikio makubwa kwa kipa yoyote wa mpira wa miguu. Rekodi hizi hutoa hadhi kwa makipa na mara nyingi humfanya kipa kutambulika kua bora kwa muda mrefu. Makipa wenye clean sheet nyingi wanaheshimika kwa uwezo wao wa kudhibiti lango dhidi ya mashambulizi ya timu pinzani. Katika ligi kubwa za Ulaya, makipa mbalimbali wamefanikiwa kuweka rekodi za clean sheets zinazovutia na kuwafanya kuwa miongoni mwa vinara wa historia ya soka. Hapa chini tunakuletea orodha ya baadhi ya makipa waliofanikiwa kuweka clean sheets nyingi katika msimu mmoja katika ligi kuu barani Ulaya.
Jedwali la Vinara wa Clean Sheets Ulaya
Jina la Kipa | Clean Sheets (Mechi) | Timu | Msimu |
Andoni Zubizarreta | 24 | Barcelona | 1986/87 |
Jan Oblak | 24 | Atletico Madrid | 2015/16 |
Petr Cech | 24 | Chelsea | 2004/05 |
Francisco Liano | 26 | Deportivo | 1993/94 |
Marc-Andre Ter Stegen | 26 | Barcelona | 2015/16 |
1. Andoni Zubizarreta – Mechi 24 (Barcelona, 1986/87)
Andoni Zubizarreta, maarufu kama “Zubi,” alikuwa kipa wa Barcelona msimu wa 1986/87 ambapo aliweka clean sheets kwenye mechi 24 za La Liga. Ingawa Barcelona waliruhusu mabao 29 msimu huo, bado walimaliza katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi. Jitihada za Zubizarreta langoni zilikuwa nguzo muhimu kwa Barcelona, zikionesha uwezo wake wa hali ya juu.
2. Jan Oblak – Mechi 24 (Atletico Madrid, 2015/16)
Jan Oblak, raia wa Slovenia, alifahamika kwa uhodari wake akiwa na Atletico Madrid. Msimu wa 2015/16 alicheza mechi 24 bila kuruhusu bao, na hatimaye kutwaa tuzo ya Zamora. Rekodi hii ilimuweka kwenye nafasi ya juu kama mmoja wa makipa wenye mafanikio makubwa katika La Liga.
3. Petr Cech – Mechi 24 (Chelsea, 2004/05)
Petr Cech alijiunga na Chelsea msimu wa 2004/05 na haraka akaonesha uwezo wake mkubwa. Katika msimu wake wa kwanza, aliweka clean sheets kwenye mechi 24 na kusaidia Chelsea kushinda Ligi Kuu ya England baada ya miaka 50. Uwezo wake wa kudhibiti lango ulikuwa muhimu kwa mafanikio ya Chelsea msimu huo, huku akiruhusu mabao 15 tu.
4. Francisco Liano – Mechi 26 (Deportivo La Coruna, 1993/94)
Francisco Liano aliweka rekodi ya clean sheets kwenye mechi 26 akiwa na Deportivo msimu wa 1993/94, na kuruhusu mabao 18 tu msimu mzima. Rekodi hii iliweka alama mpya katika historia ya La Liga na kumpa heshima Liano kama mmoja wa makipa bora katika historia ya soka la Uhispania.
5. Marc-Andre Ter Stegen – Mechi 26 (Barcelona, 2015/16)
Marc-Andre Ter Stegen, kipa wa Barcelona, alijiwekea rekodi ya kucheza mechi 26 bila kuruhusu bao msimu wa 2015/16. Uwezo wake wa kudhibiti lango ulikuwa kiungo muhimu kwa mafanikio ya Barcelona, huku kikosi hicho kikiruhusu mabao 15 tu msimu mzima. Rekodi hii inabaki kuwa mojawapo ya rekodi kubwa zaidi kwa kipa katika historia ya La Liga.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Kikosi cha Azam Fc Vs Yanga SC Leo 02 Novemba 2024
- Kikosi cha Yanga Vs Azam Fc Leo 02/11/2024
- Yanga Vs Azam Fc Leo 02/11/2024 Saa Ngapi?
- Ratiba ya Mechi za Leo Ligi Kuu ya NBC Tanzania 02/11/2024
- Ratiba ya Mechi za Leo 02/11/2024
- Fountain Gate Yajiandaa Kuikabili Pamba FC Novemba 5
- Sopu Kubaki Chamanzi Hadi 2025/2026
Leave a Reply