Orodha ya Timu Tajiri Duniani 2024

Orodha ya Timu Tajiri Duniani 2024 | Timu Zinazoongoza Kwa Pesa Duniani

Mchezo wa soka umekuwa ukivutia mashabiki na wawekezaji wengi kote duniani, jambo ambalo limepelekea timu nyingi soka duniani kujikusanjia mamilioni ya dola za kimarekani kutokea kwenye vyanzo mbalimbali ambavyo miongoni mwa vyanzo hivyo ni mauzo ya jezi, haki za matangazo, zawadi za kushinda michuano mbalimbali n.k. Kwa mwaka wa 2024, orodha ya timu tajiri zaidi duniani imekuwa na mabadiliko kadhaa huku timu nyingi zikiongeza mapato yao kutokana na mikataba ya kibiashara, haki za matangazo, na mapato ya mechi.

Katika orodha hii, tunachunguza klabu tajiri zaidi duniani kwa mapato ya mwaka huu, tukiongozwa na Real Madrid, ambayo imechukua nafasi ya kwanza baada ya kufikisha mapato ya juu zaidi.

  1. Real Madrid – £714.7 million
  2. Manchester City – £709.9 million
  3. Paris Saint-Germain – £689.2 million
  4. Barcelona – £687.6 million
  5. Manchester United – £640.1 million
  6. Bayern Munich – £639.5 million
  7. Liverpool – £587 million
  8. Tottenham Hotspur – £542.8 million
  9. Chelsea – £506.3 million
  10. Arsenal – £457.8 million
  11. Juventus – £371.7 million
  12. Borussia Dortmund – £361 million
  13. AC Milan – £331.2 million
  14. Internazionale – £325.7 million
  15. Atletico Madrid – £313 million
  16. Eintracht Frankfurt – £252.3 million
  17. Newcastle United – £247.4 million
  18. West Ham United – £236.5 million
  19. Napoli – £230.1 million
  20. Marseille – £222.1 million

Orodha ya Timu Tajiri Duniani 2024

1. Real Madrid – £714.7 milioni

Real Madrid imefanikiwa kurejea kileleni kama timu tajiri zaidi duniani kwa mwaka 2024, ikiwapita Manchester City. Mkataba wa kibiashara na kampuni ya teknolojia ya HP umeongeza mapato yao kwa kiwango kikubwa. Pia, klabu imeendelea kuvutia mashabiki kupitia mapato ya mechi, jambo ambalo limeongeza kwa asilimia 8 ikilinganishwa na msimu uliopita.

Tangu mwaka wa 2004-2005, Real Madrid imekuwa ikishikilia nafasi ya kwanza katika orodha hii mara nyingi, na kuonyesha ustahimilivu wao kifedha licha ya ushindani kutoka kwa klabu zingine kubwa.

2. Manchester City – £709.9 milioni

Manchester City, mabingwa wa trebo ya mwaka 2022-2023, wameweka rekodi mpya ya mapato baada ya kufikia kiasi cha £709.9 milioni. Mafanikio yao uwanjani, pamoja na mipango madhubuti ya kibiashara, imewafanya kuwa klabu yenye nguvu ya kifedha duniani. Ingawa mapato yao ya siku ya mechi ni madogo ukilinganisha na wapinzani wao, City imeendelea kung’ara katika medani ya kimataifa.

3. Paris Saint-Germain (PSG) – £689.2 milioni

PSG imepata mapato makubwa licha ya kupoteza wachezaji nyota kama Lionel Messi, Neymar, na Kylian Mbappé katika kipindi cha miaka 18 iliyopita. Hata hivyo, klabu imepata hasara kwa mwaka wa tatu mfululizo. Mikakati ya uendeshaji wa timu hii ya Ufaransa inaweza kubadilika katika miaka ijayo, na kuna uvumi wa mabadiliko ya umiliki katika klabu hiyo.

4. Barcelona – £687.6 milioni

Barcelona imeongeza mapato yake kwa kiwango kikubwa baada ya kupitia changamoto za kifedha katika miaka ya karibuni. Uhamisho wa Lionel Messi na matatizo ya kifedha yaliyowakumba, yaliathiri mapato yao, lakini mkataba mpya wa tiketi na uwanja wa michezo wa Olimpiki umechangia kuimarisha kipato cha klabu. Uwanja wa Camp Nou, unaoendelea kufanyiwa ukarabati, unatarajiwa kuwa rasilimali kubwa kwao katika nusu ya pili ya muongo huu.

5. Manchester United – £640.1 milioni

Manchester United imeendelea kuwa moja ya timu tajiri zaidi licha ya changamoto za uwanjani. Pamoja na kuwepo kwa mgogoro wa wamiliki na mashabiki, klabu imefanya vizuri kibiashara, hasa baada ya uwekezaji wa Jim Ratcliffe na INEOS. Manchester United ina nafasi kubwa ya kurejea kileleni kifedha iwapo itafanikiwa kurudi kwa kasi kwenye mashindano makubwa kama Ligi ya Mabingwa.

6. Bayern Munich – £639.5 milioni

Bayern Munich imeendelea kuwa klabu yenye mapato ya kibiashara makubwa zaidi duniani, kutokana na ushirikiano wake wa muda mrefu na kampuni ya simu ya T-Mobile. Hata hivyo, mapato yao ya matangazo ya moja kwa moja hayalingani na klabu za Ligi Kuu ya Uingereza, lakini mafanikio ya uwanjani na kibiashara yamewaweka juu kwenye orodha hii.

7. Liverpool – £587 milioni

Liverpool imeimarisha mapato yake kupitia mikataba mipya ya udhamini na makampuni kama AXA, Carlsberg, na Google. Ingawa walishuka kidogo kifedha kutoka nafasi yao ya awali, klabu inayo msingi thabiti kifedha na inaendelea kuvutia wawekezaji. Mafanikio ya uwanjani na ushirikiano wa kibiashara unaweka Liverpool katika nafasi nzuri kwa miaka ijayo.

8. Tottenham Hotspur – £542.8 milioni

Tottenham Hotspur, licha ya kukosa nafasi ya kushiriki mashindano ya Ulaya kwa msimu wa 2023-2024, wameendelea kujipatia mapato mazuri, hasa kutokana na uwanja wao mpya. Uwanja huu umekuwa na mchango mkubwa, huku asilimia 20 ya mapato yao ikitokana na mapato ya siku ya mechi.

9. Chelsea – £506.3 milioni

Chelsea wanakabiliwa na changamoto za kifedha chini ya uongozi mpya wa Todd Boehly. Mikataba ya udhamini imekuwa gumzo, huku kampuni ya Infinite Athlete ikichukua nafasi kwenye jezi zao kwa msimu wa 2023-2024. Hata hivyo, Chelsea wanahitaji kufanya vizuri uwanjani ili kuendelea kuvutia mapato ya matangazo na kibiashara.

10. Arsenal – £457.8 milioni

Arsenal imeshika nafasi ya kumi katika orodha hii. Mkataba mpya wa udhamini na Fly Emirates umeongeza mapato yao, huku klabu ikirudi kushindana katika Ligi Kuu ya Uingereza na Ligi ya Mabingwa. Thamani ya klabu imepanda kwa asilimia 15 ndani ya miezi 12 iliyopita, jambo linalodhihirisha nguvu ya kifedha ya soka la Uingereza.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Dickson Job: Fedha za Goli la Mama Zinatupandisha Morali
  2. Gamondi Asema Hakuna wa Kumtisha Makundi Klabu Bingwa
  3. Wachezaji Sita wa Uingereza Watajwa Kwenye Orodha ya Ballon d’Or 2024
  4. Orodha ya Matajiri 10 Duniani 2024
  5. Orodha ya Makocha Timu za Ligi Kuu ya NBC 2024/2025
  6. Orodha Ya Vyuo Bora Tanzania 2024
  7. Orodha ya Mabingwa wa Kombe La Shirikisho Tanzania
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo