NECTA Matokeo ya Kidato Cha Pili 2024 | Matokeo ya Form Two 2024/2025 (NECTA Form Two Results FTNA)
Mtihani wa Upimaji wa Kidato cha Pili, almaarufu kama Form Two National Assessment (FTNA), ni mojawapo ya mitihani muhimu inayosimamiwa na Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) na kufanywa na shule zote za sekondari Tanzania.
Mtihani huu hufanyika kila mwaka kwa wanafunzi wa shule za sekondari kote nchini Tanzania. Lengo kuu la FTNA ni kutathmini uelewa wa wanafunzi baada ya miaka miwili ya masomo ya sekondari na kutoa mrejesho muhimu kwa walimu, wanafunzi, na wadau wa elimu kwa lengo la kuboresha mbinu za kufundisha na kujifunza.
Mtihani huu unahusisha masomo mbalimbali yanayochangia maendeleo ya kitaaluma ya wanafunzi. Masomo haya ni pamoja na:
- Kiswahili
- Basic Mathematics
- English Language
- Biolojia
- Fizikia
- Kemia
- Jiografia
- Historia
- Elimu ya Dini ya Kiislamu
- Bible Knowledge
- Uraia
- Masomo ya Ufundi kama Building Construction, Mechanical Engineering, na Electrical Engineering
- Masomo ya Biashara kama Book-Keeping na Commerce
- Lugha za Kigeni kama Kifaransa na Kichina
Kwa mujibu wa NECTA, matokeo haya yana umuhimu mkubwa kwa sababu hutoa mwelekeo wa kitaaluma kwa wanafunzi, ikiwezekana kuwasaidia kubainisha nguvu na changamoto zao kabla ya kuendelea na Kidato cha Tatu.
NECTA Matokeo ya Kidato Cha Pili 2024 (Form Two Results)
Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) limetangazoa matokeo ya mtihani wa upimaji wa Kidato cha Pili leo Jumamosi, Januari 4, 2025. Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa na NECTA, jumla ya wanafunzi 680,574 kati ya wanafunzi 796,825 waliofanya mtihani huo wamefaulu, sawa na asilimia 85.41.
Matokeo haya yanaonyesha kuwa wasichana waliokuwa na mafanikio ni 367,457, wakichangia asilimia 54, huku wavulana wakiwa 313,117, sawa na asilimia 46.
Tunaelewa umuhimu wa matokeo haya kwa wanafunzi, wazazi, na walezi. Kwa hivyo, hapa tutakuelekeza hatua kwa hatua jinsi ya kuangalia matokeo ya Kidato cha Pili 2024 kwa urahisi na haraka mara tu yanapotangazwa. Pia, tutakupa viungo vya moja kwa moja vya tovuti ya NECTA na njia zingine rasmi za kupata matokeo haya ili kuepuka upotoshaji wa taarifa.
Endelea kufuatilia ukurasa huu kwa taarifa za kina na sasisho kuhusu matokeo ya Kidato cha Pili 2024. Tunajitahidi kuhakikisha unapata habari sahihi na kwa wakati.
Jinsi ya Kuangalia Matokeo ya Kidato cha Pili 2024 Mtandaoni
Matokeo ya Kidato cha Pili yanaweza kupatikana kwa urahisi kupitia tovuti rasmi ya NECTA. Ufuatao ni mwongozo kamili wenye hatua za kufuata ili kuangalia matokeo ya mtihani wa upimaji wa kidato cha pili 2024 (NECTA Form two results)
1. Tembelea Tovuti Rasmi ya NECTA
Fungua kivinjari cha intaneti na tembelea tovuti rasmi ya NECTA kwa anwani www.necta.go.tz. Ni muhimu kuhakikisha mtandao wako wa intaneti ni imara ili kuepuka matatizo ya upakiaji wa kurasa.
2. Chagua Sehemu ya “Results” (Matokeo ya Mitihani)
Baada ya kufungua tovuti, bofya kitufe cha Results kinachoonekana kwenye menyu kuu. Hii itakufikisha kwenye orodha ya mitihani yote inayosimamiwa na NECTA.
3. Chagua “FTNA” (Form Two National Assessment)
Kutoka kwenye orodha ya mitihani, tafuta FTNA, ambayo inawakilisha matokeo ya Kidato cha Pili. Bonyeza ili kufungua ukurasa wa matokeo hayo.
4. Chagua Mwaka wa Mtihani
Baada ya kufungua ukurasa wa FTNA, utaona miaka ya matokeo iliyoorodheshwa. Tafuta na chagua mwaka husika, yaani, 2024.
5. Tafuta Jina la Shule
Mara baada ya kuchagua mwaka, utaelekezwa kwenye orodha ya shule zote zilizoshiriki mtihani huo. Tumia kipengele cha utafutaji kutafuta jina la shule yako ili kuonyesha matokeo ya wanafunzi wote wa shule hiyo.
6. Tafuta Jina la Mwanafunzi au Namba ya Mtihani
Baada ya kubofya jina la shule, utaona orodha ya wanafunzi wote waliofanya mtihani katika shule husika pamoja na matokeo waliyopata. Kujua matokeo ya mwanafunzi mmoja tafuta jina la mwanafunzi huyo au namba ya mtihani kwa kutumia kipengele cha utafutaji (Ctrl+F kwa kompyuta). Matokeo yatakayoonekana yatakuwa na:
- Jina la mwanafunzi
- Alama za kila somo
- Jumla ya alama
- Daraja la ufaulu (Division).
Angalizo Muhimu: Ili kuhakikisha upatikanaji wa matokeo sahihi, ni vyema kutumia vyanzo rasmi pekee, kama tovuti ya NECTA. Epuka tovuti zisizoaminika ambazo zinaweza kutoa taarifa zisizo sahihi au za kupotosha. Ikiwa unakutana na changamoto yoyote, unashauriwa kuwasiliana moja kwa moja na shule yako au ofisi za NECTA kwa msaada wa haraka.
ANGALIA MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024 MOJA KWA MOJA HAPA
ARUSHA | MOROGORO |
DAR ES SALAAM | MTWARA |
DODOMA | MWANZA |
GEITA | NJOMBE |
IRINGA | PWANI |
KAGERA | RUKWA |
KATAVI | RUVUMA |
KIGOMA | SHINYANGA |
KILIMANJARO | SIMIYU |
LINDI | SINGIDA |
MANYARA | SONGWE |
MARA | TABORA |
MBEYA | TANGA |
Umuhimu wa Matokeo ya Kidato cha Pili
Matokeo haya si tu yanatumika kama kipimo cha maendeleo ya kitaaluma, bali pia yanaathiri maamuzi ya kitaaluma kwa wanafunzi. Wanafunzi waliofanikiwa kwa alama nzuri wana nafasi nzuri zaidi ya kuchagua masomo maalum pindi wanapoanza masomo ya Kidato cha Tatu, kama vile Sayansi, Biashara, au Sanaa. Aidha, matokeo haya huwasaidia walimu kutathmini ufanisi wa mbinu za kufundisha.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Jinsi ya Kuangalia matokeo ya Darasa la Nne 2024
- Majina ya Wanafunzi na Shule Walizopangiwa Kidato cha Kwanza 2025
- Matokeo ya Darasa la Nne 2024 Mkoa wa Dodoma
- Matokeo ya Darasa la Nne 2024 Mkoa wa Tanga
- Jinsi ya Kuangalia Matokeo ya Kidato Cha Pili 2024
- Matokeo ya Darasa la Nne 2024 Mkoa wa Kigoma
- Matokeo ya Darasa la Nne 2024 Iringa
- Matokeo ya Darasa la Nne 2024 Tabora
- Matokeo ya Darasa la Nne 2024 Mkoa wa Rukwa
- Matokeo ya Darasa la Nne 2024 Mbeya
Leave a Reply