NECTA: Matokeo ya Kidato cha Nne 2024 | Matokeo ya Form Four 2024/2025
Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) leo tarehe 23 Januari 2025 limetangaza matokeo ya mtihani wa kitaifa wa kuhitimu elimu ya sekondari, maarufu kama mtihani wa kidato cha nne. Mtihani huu, uliofanyika kati ya tarehe 11 Novemba 2024 hadi 29 Novemba 2024, umewashuhudia watahiniwa 477,262 kati ya 516,695 waliofanya mtihani wakifaulu kwa kupata madaraja ya I, II, III na IV.
NECTA imesema kuwa ufaulu huu umepanda kwa asilimia 3, na kufikia asilimia 92.37 kutoka asilimia 89.36 mwaka 2023. Hii inaashiria kuimarika kwa kiwango cha elimu nchini.
Kwa mujibu wa NECTA, idadi ya watahiniwa waliopata madaraja ya I, II na III imeongezeka na kufikia 221,953 sawa na asilimia 43, ikilinganishwa na mwaka 2023 ambapo idadi ilikuwa 197,426 sawa na asilimia 37.4. Huku idadi ya watahiniwa waliopata daraja la IV na sifuri ikipungua, ubora wa ufaulu umepanda kwa asilimia 5.6.
Wasichana Waongoza kwa Idadi, Wavulana kwa Ubora
Katika watahiniwa 477,262 waliofaulu, wasichana ni 249,078 sawa na asilimia 52, na wavulana ni 228,184 sawa na asilimia 48. Hata hivyo, kwa kuangalia ubora wa ufaulu wa jinsia, kwa kuzingatia ufaulu wa madaraja ya I-III, wavulana wameongoza kwa kupata asilimia 54 (119,869) huku wasichana wakipata asilimia 46 (102,084).
Lengo la Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE)
Mtihani wa Kidato cha Nne unalenga kutathmini ujuzi na maarifa yaliyopatikana na mwanafunzi katika masomo mbalimbali ya sekondari. Huu ni mtihani wa kitaifa unaoweka vipimo vya kiwango cha elimu ya mwanafunzi na uwezo wake wa kutumia ujuzi alioupata katika kutatua changamoto mbalimbali za kijamii, kisiasa, kiuchumi, na kiteknolojia. Aidha, mtihani huu unasaidia kubaini wanafunzi wanaohitaji kuendelea na elimu ya juu au kujiunga na vyuo vya ufundi.
Masomo Yanayojumuishwa katika Mtihani wa Kidato cha Nne
Kila mwanafunzi atakayejiandikisha kwa mtihani wa Kidato cha Nne lazima afanye mitihani ya masomo saba ya msingi, ambayo ni:
- Civics
- Historia
- Geografia
- Kiswahili
- Kingereza
- Biolojia
- Hisabati ya Msingi
Aidha, wanafunzi wanaweza kuchagua masomo ya ziada kutoka katika makundi mbalimbali kama vile Sayansi ya Asili (Fizikia na Kemia), Masomo ya Biashara (Biashara na Uhasibu), au masomo ya Ufundi kama vile Ujenzi, Usanifu, na Utengenezaji wa Vifaa mbalimbali vya Kielektroniki. Wanafunzi pia wanaweza kuchagua masomo ya kidini, Sanaa, Michezo, au Kiswahili cha Kiufundi.
Lini Matokeo ya Kidato cha Nne 2024 Yanatarajiwa Kutangazwa?
Hadi sasa, Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) halijatoa taarifa rasmi kuhusu tarehe ya kutangazwa kwa matokeo ya Kidato cha Nne 2024. Hata hivyo, kutokana na desturi za mwaka jana na miaka mingine iliyopita, ni wazi kwamba matokeo haya yanatarajiwa kutangazwa mwezi Januari 2024. Kwa mfano:
- 2023: Matokeo ya Kidato cha Nne yalitangazwa Januari 25.
- 2022: Matokeo yalitangazwa Januari 29.
- 2021: Matokeo yalitangazwa Januari 15.
- 2020: Matokeo yalitangazwa Januari 15.
Kwa hivyo, tunatarajia kuwa matokeo ya mwaka huu yatatangazwa katikati mwa Januari 2025.
Jinsi ya Kuangalia Matokeo ya Kidato cha Nne 2024 Kupitia Tovuti ya NECTA
Katika zama hizi za kiteknolojia, kupata matokeo ya mtihani wa Kidato cha Nne ni rahisi na salama kupitia tovuti rasmi ya NECTA. Hapa chini ni hatua za kufuata ili kupata matokeo yako:
- Tembelea Tovuti Rasmi ya NECTA
Ili kupata matokeo yako, tafadhali nenda kwenye tovuti rasmi ya NECTA kwa kuandika anwani ya www.necta.go.tz katika kivinjari (browser) chako. - Tafuta Sehemu ya Matokeo
Mara utakapofika kwenye tovuti ya NECTA, tafuta sehemu ya “Results” au “Matokeo” katika menyu kuu. Hii itakupeleka kwenye orodha ya matokeo ya mitihani mbalimbali.
- Chagua Aina ya Mtihani
Katika orodha ya matokeo, chagua “CSEE” ili kuona matokeo ya Kidato cha Nne. - Chagua Linki ya Matokeo ya Mwaka 2024
Katika ukurasa wa matokeo ya Kidato cha Nne, utaona orodha ya matokeo ya miaka tofauti. Bonyeza linki ya mwaka 2024 ili kupata matokeo ya mtihani huo. - Tafuta Shule uliyosoma
Baada ya kufungua ukurasa wa matokeo ya Kidato cha Nne 2024, tafuta jina la shule yako ili kuona matokeo. Unaweza pia kutafuta matokeo kwa kutumia namba yako ya mtihani (Index Number).
- Angalia na Pakua Matokeo
Matokeo yako yatakuja kwenye skrini. Unaweza kuyachapisha au kuyahifadhi kwenye kifaa chako cha kompyuta au simu kwa matumizi ya baadaye.
Angalia Matokeo ya Kidato cha Nne Kupitia Viungo hapa chini
Kuelewa Matokeo ya Kidato cha Nne kwa Kina
Matokeo ya Kidato cha Nne ni moja ya alama muhimu zinazoweka msingi wa mwelekeo wa taaluma na maisha ya wanafunzi. Matokeo haya hupatikana baada ya kufanyika kwa Mtihani wa kitaifa wa Kuhitimu Elimu ya Sekondari (CSEE), unaoandaliwa na kusimamiwa na Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA). Matokeo haya huonyesha si tu ufaulu wa wanafunzi mmoja mmoja, bali pia kiwango cha ufaulu wa shule kwa ujumla, na ni rejeleo la msingi kwa wadau wa elimu kufanya maamuzi.
Muundo wa Matokeo ya Kidato cha Nne
Matokeo ya Kidato cha Nne yana vipengele muhimu vinavyosaidia kuelewa viwango vya ufaulu wa mwanafunzi na shule kwa ujumla. Vipengele hivi ni pamoja na:
Taarifa za Jumla:
- Shule na Namba ya Kituo: Kila shule inatambulishwa kwa jina na namba ya kituo.
- Idadi ya Watahiniwa: Inaonyesha idadi ya wanafunzi waliosajiliwa, walioketi mtihani, na waliokosa.
- Daraja la Kila Mwanafunzi: Madaraja yanatolewa kutoka Division I hadi Division 0.
Madaraja ya Ufaulu:
- Division I: Linaonyesha ufaulu wa hali ya juu sana, ambapo mwanafunzi hupata wastani wa alama bora kwenye masomo yake yote.
- Division II: Ufaulu wa kiwango cha juu lakini chini kidogo ya Division I.
- Division III: Ufaulu wa wastani.
- Division IV: Ufaulu wa kiwango cha chini.
- Division 0: Mwanafunzi aliyeshindwa au aliyekosa kufikia viwango vya ufaulu.
Alama za Masomo Binafsi: Kila mwanafunzi hupimwa kwenye masomo tofauti, na matokeo yao yanaonyeshwa kwa daraja kama vile A (bora kabisa), B, C, D, na F (kushindwa). Kwa mfano, mwanafunzi anaweza kuwa na:
- Kiswahili: A
- Kiingereza: C
- Baiolojia: D
GPA ya Shule:
Shule hupata wastani wa ufaulu unaojulikana kama Grade Point Average (GPA), ambao unajumuisha matokeo ya watahiniwa wote. GPA ya chini inaonyesha ufaulu wa hali ya juu, huku ya juu ikiashiria changamoto za kitaaluma.
Tathmini ya Masomo ya Shule:
Masomo kama Hisabati, Kiswahili, Historia, Fizikia, na Baiolojia yanapimwa kwa viwango tofauti vya ufaulu wa shule. Masomo yenye changamoto mara nyingi hupewa daraja la chini zaidi, kama F (Fail), huku masomo yaliyoimarika yakipata daraja bora, kama A au B.
Umuhimu wa Matokeo ya NECTA Kidato cha Nne
Matokeo haya ni kiashiria muhimu cha maendeleo ya taaluma ya mwanafunzi na shule. Hufanikisha mambo yafuatayo:
Kuamua Hatua ya Mbele ya Masomo:
- Wanafunzi waliopata madaraja bora (Division I na II) wana nafasi nzuri ya kujiunga na shule za kidato cha tano au vyuo vya kati vya kitaaluma.
- Wale wenye Division III na IV wanaweza kujiunga na mafunzo ya ufundi au masomo ya vyuo vya kawaida.
Tathmini ya Nguvu na Udhaifu:
- Matokeo hutoa mwanga kuhusu maeneo ambayo mwanafunzi ana nguvu au anahitaji kuboresha. Kwa mfano, mwanafunzi aliyepata A katika Fizikia lakini D katika Baiolojia anapaswa kuelekeza juhudi zaidi kwenye masomo ya sayansi ya uhai.
Tathmini ya Ufanisi wa Shule:
- Wadau wa elimu, kama serikali na wazazi, hutumia matokeo haya kutathmini ufanisi wa shule. Shule yenye GPA bora inaweza kuonekana kuwa na mifumo bora ya kufundisha, ilhali yenye GPA ya juu inaweza kuhitaji maboresho.
Maamuzi ya Kitaaluma:
- Wanafunzi wanaweza kutumia matokeo yao kuamua ni taaluma gani itakayowafaa kulingana na matokeo yao. Kwa mfano, ufaulu mzuri katika masomo ya biashara unaweza kumwelekeza mwanafunzi kuchagua taaluma ya biashara au uhasibu.
Changamoto Zinazoathiri Matokeo ya Kidato cha Nne Kwa Wanafunzi
Changamoto zinazoweza kuathiri matokeo ya wanafunzi ni pamoja na:
- Uhaba wa Walimu: Hii huathiri ufanisi wa ufundishaji, hasa katika masomo ya sayansi.
- Vifaa Duni vya Kujifunzia: Kutokuwepo kwa maabara au vitabu vya kiada vya kutosha kunapunguza nafasi za ufaulu.
- Utoro wa Wanafunzi: Kutokuhudhuria masomo kwa muda mrefu huathiri uwezo wa mwanafunzi kushiriki mtihani kikamilifu.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Matokeo Kidato cha Nne 2024 Yanatoka Lini? (NECTA Results)
- Jinsi ya Kuangalia Matokeo ya Kidato Cha Nne 2024
- Shule Walizopangiwa Darasa la Saba 2025
- Matokeo ya Darasa la Nne 2024/2025 (NECTA Standard Four Results)
- Matokeo ya Darasa la Nne 2024 NECTA
- NECTA Matokeo ya Kidato Cha Pili 2024 (Form Two Results)
- Majina ya Wanafunzi na Shule Walizopangiwa Kidato cha Kwanza 2025
- Majina ya Waliochaguliwa Kidato cha Kwanza 2025
Leave a Reply