Ndoa Ya Coastal na Ley Matampi Yavunjika Rasmi

Ndoa Ya Coastal na Ley Matampi Yavunjika Rasmi

Ndoa Ya Coastal na Ley Matampi Yavunjika Rasmi

Uongozi wa Coastal Union umethibitisha rasmi kuvunjika kwa mkataba wa kipa wao maarufu, Ley Matampi, ambaye alionyesha kiwango cha juu msimu uliopita na kuchangia kwa kiasi kikubwa mafanikio ya timu hiyo. Taarifa rasmi kutoka kwa klabu hiyo ilitolewa siku ya Jumanne, Desemba 10, 2024, ikisema kwamba pande zote mbili zimefikia makubaliano ya kumaliza mkataba wa kipa huyo, ambaye alijiunga na Coastal Union Agosti 2023 akitokea Jeunesse Sportive Groupe Bazano ya DR Congo.

Matampi, aliyeshinda Tuzo ya Kipa Bora wa Ligi Kuu Bara msimu uliopita wa 2023/2024, alijiunga na Coastal Union mnamo Agosti 2023 akitokea Jeunesse Sportive Groupe Bazano ya DR Congo. Hata hivyo, uongozi wa Coastal Union umetangaza rasmi kuvunjika kwa mkataba wake, baada ya makubaliano ya pande zote mbili.

Taarifa rasmi ya klabu iliyotolewa Desemba 10, 2024, imesema: “Tumefikia makubaliano baina ya klabu yetu na kipa Ley Matampi ya kumaliza huduma za pande zote mbili. Uzoefu wako umechangia kwa asilimia kubwa mafanikio yetu ya msimu uliopita. Shukrani za kipekee kwa kocha wa magolikipa Mansour Ally ambaye alitumia nguvu kubwa ya kurudisha uwezo na kiwango chako ukawa msaada mkubwa eneo la kulinda lango letu. Tunakutakia kheri nyingi na mafanikio zaidi katika maisha yako.”

Ndoa Ya Coastal na Ley Matampi Yavunjika Rasmi

Mchango wa Matampi kwa Coastal Union

Matampi alicheza kwa kiwango cha juu, akimaliza msimu uliopita akiwa na clean sheet 15, rekodi iliyomfanya kuwa kinara wa ligi. Uwezo wake mkubwa uliisaidia Coastal Union kumaliza katika nafasi ya nne kwenye Ligi Kuu Bara, hatua iliyowapa nafasi ya kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu huu.

Akizungumzia kuvunjika kwa mkataba wake, Matampi alisema:

“Nilipewa barua wiki iliyopita na kwangu naona ni uamuzi mzuri tu ambao klabu imefikia.”

Kwa Coastal Union, kuvunjika kwa mkataba wa Matampi ni sehemu ya mabadiliko ya klabu hiyo kuelekea msimu ujao. Kwa mchango wake wa kipekee msimu uliopita, Matampi anaacha alama kubwa katika historia ya timu hiyo na moyo wa shukrani kutoka kwa uongozi na mashabiki.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Mapinduzi Cup 2025 Kuchezwa na Timu za Taifa Badala ya Vilabu
  2. Kocha Ramovic Aeleza Sababu za Yanga Kushindwa Mbele ya Waarabu
  3. Yanga Karibu Kumsajili Kelvin Nashon kutoka Singida
  4. Habib Kyombo Ajiunga na Pamba Jiji Kwa Mkopo
  5. Shabani Pandu na Mudrik Abdi Gonda Mbiuoni Kujiunga Fountain Gate
  6. Simba Yachezea Chuma 2-1 Dhidi ya CS Constantine
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo