Morocco vs Tanzania (Taifa Stars) Leo 25/03/2025 Saa Ngapi?

Morocco vs Tanzania Taifa Stars Leo Saa Ngapi

Morocco vs Tanzania (Taifa Stars) Leo 25/03/2025 Saa Ngapi?

Kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania, almaarufu kama Taifa Stars, leo kitashuka dimbani kumenyana na miamba wa soka barani Afrika, Morocco, katika mchezo wa kuwania tiketi ya kufuzu Kombe la Dunia la mwaka 2026. Mchezo huu muhimu unatarajiwa kuanza saa 6:30 usiku kwa saa za Tanzania, na utapigwa katika dimba la Stade Municipal.

Mchezo huu ni wa hatua ya makundi ya kufuzu kwa Kombe la Dunia 2026 kwa upande wa CAF. Morocco, ambayo imeonyesha kiwango cha juu kwenye mechi zilizopita, inaongoza kundi E kwa alama zote tisa baada ya kushinda michezo yao yote mitatu.

Taifa Stars, kwa upande wao, wamefanikiwa kushinda michezo miwili kati ya mitatu waliocheza, jambo linalowaweka kwenye nafasi nzuri ya kupambana kupata matokeo mazuri dhidi ya wenyeji wao.

Morocco vs Tanzania (Taifa Stars) Leo 25/03/2025 Saa Ngapi?

Formu ya Timu zote Mbili

Morocco inakuja kwenye mchezo huu ikiwa na morali ya juu baada ya kuendeleza rekodi yao ya ushindi kwa mechi tisa mfululizo katika mashindano yote. Ushindi wao wa hivi karibuni ulikuwa dhidi ya Niger, ambapo walitoka nyuma na kushinda 2-1 kwa mabao ya Ismael Saibari na Bilal El Khannouss. Taifa Stars, kwa upande wao, hawakucheza mchezo wowote wiki iliyopita baada ya mechi yao dhidi ya Congo kufutwa kufuatia kufungiwa kwa Shirikisho la Soka la Congo (FECOFOOT) na FIFA. Mechi yao ya mwisho ilikuwa Januari walipopoteza 2-0 dhidi ya Burkina Faso katika mchezo wa kirafiki.

Historia ya Mikutano Kati ya Timu Hizi

Katika mechi sita zilizopita kati ya Morocco na Tanzania, matokeo yamekuwa yakipendelea Morocco, ambao wameshinda mara tano huku Taifa Stars wakishinda mara moja pekee. Vilevile, Morocco wamekuwa na rekodi bora zaidi nyumbani, wakishinda michezo minne mfululizo kwenye mashindano rasmi huku wakihifadhi nyavu zao mara mbili mfululizo.

Taifa Stars wataingia katika mchezo huu wakijivunia rekodi nzuri ya kutopoteza katika mechi zao sita za ugenini kwenye hatua ya kufuzu Kombe la Dunia, huku wakishinda tatu kati ya hizo.

Takwimu Muhimu Zinazobeba Mchezo Huu

  • Morocco imepata ushindi katika michezo yote mitatu ya kundi E.
  • Taifa Stars imeshinda michezo miwili kati ya mitatu kwenye kundi E, na ushindi wote wameupata ugenini.
  • Morocco haijapoteza katika michezo 18 ya kufuzu Kombe la Dunia.
  • Tanzania haijapoteza katika mechi zao sita za mwisho za ugenini kwenye hatua ya kufuzu, huku wakifunga bao moja katika kila mechi.
  • Morocco imefunga mabao mawili au zaidi katika mechi zao tano zilizopita dhidi ya Tanzania.
  • Timu tatu pekee (Misri, Burkina Faso na Ivory Coast) ndizo zilizofunga mabao mengi zaidi (13) kuliko Morocco (12) kwenye hatua ya kufuzu.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Ufunguzi wa Uwanja Mpya wa Singida Black Stars Wavurugwa na Mvua Kubwa
  2. Salum Mayanga Aanza Rasmi Majukumu Kama Kocha Mkuu wa Mashujaa FC
  3. Mechi ya Kirafiki ya Singida Black Stars Vs Yanga Leo 24/03/2025 Saa Ngapi
  4. Thiago Motta Atumbuliwa Juventus, Igor Tudor Atangizwa Kocha Mpya
  5. Gomez Aanza Kuingia Kwenye Mfumo wa Wydad Baada ya Mapambano ya Awali
  6. Ibrahima Konate Ndani ya Rada za PSG
  7. Refa ‘Nuksi’ Achaguliwa Kuchezesha Mechi ya Taifa Stars Dhidi ya Morocco
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo