Mbeya City Yaing’oa Azam CRDB Bank Federation Cup kwa Mikwaju ya Penati

Mbeya City Yaingoa Azam CRDB Bank Federation Cup kwa Mikwaju ya Penati

Mbeya City Yaing’oa Azam CRDB Bank Federation Cup kwa Mikwaju ya Penati

Azam FC imeshindwa kusonga mbele katika michuano ya CRDB Bank Federation Cup baada ya kutolewa kwa mikwaju ya penalti 4-2 na Mbeya City katika mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Azam Complex, Chamazi. Timu hizo zilimaliza dakika 90 kwa sare ya mabao 1-1, hivyo kulazimika kupigiana penalti kuamua mshindi.

Mchezo huo wa hatua ya 32 bora ulianza kwa kasi, huku timu zote zikionyesha uwezo mkubwa wa kushambuliana. Mbeya City, ambayo kwa sasa inakiwasha katika ligi daraja la kwanza, ilionyesha ushindani mkali dhidi ya wana Rambaramba Azam FC, moja ya timu zinazofanya vizuri katika Ligi Kuu Tanzania Bara.

Mabao ya mchezo huo yalifungwa na Lukandamila dakika ya 65 kwa upande wa Mbeya City, kabla ya Yahya Zayd kusawazisha kwa Azam FC dakika za nyongeza (90+4). Sare hiyo ilipeleka mchezo kwenye hatua ya mikwaju ya penalti ili kumpata mshindi.

Katika mikwaju ya penalti, Mbeya City ilionyesha utulivu na umakini mkubwa, huku wachezaji wake wakifunga penalti nne kati ya tano walizopiga. Kwa upande wa Azam FC, walifanikiwa kufunga penalti mbili pekee, huku wakikosa mbili, hali iliyowapa Mbeya City nafasi ya kutinga hatua ya 16 bora.

Matokeo ya Penalti

  • Azam FC: ✅✅❌❌
  • Mbeya City: ✅✅❌✅✅

Mbeya City Yaing'oa Azam CRDB Bank Federation Cup kwa Mikwaju ya Penati

Mbeya City Yatinga Hatua ya 16 Bora

Kwa ushindi huo, Mbeya City imejihakikishia nafasi katika hatua ya 16 bora ya michuano ya CRDB Bank Federation Cup. Ushindi huu ni wa kihistoria kwa timu hiyo kwani imetolewa timu yenye uzoefu mkubwa kwenye mashindano ya ndani.

Kwa upande wa Azam FC, kutolewa mapema katika michuano hii ni pigo kubwa kwao, ikizingatiwa kwamba walikuwa na matarajio makubwa ya kusonga mbele na kutwaa taji. Mashabiki wa Azam FC watakuwa na maswali mengi kuhusu sababu za kushindwa kuhimili presha ya Mbeya City na kushindwa kutekeleza majukumu yao kwenye mikwaju ya penalti.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Ratiba ya Mechi za Simba Machi 2025
  2. Simba Yaivuruga Rekodi ya Mwambusi Arusha
  3. Amrouche Atangazwa Kocha Mpya wa Timu ya Taifa ya Rwanda
  4. Baraka Majogoro Karibu Kujiunga na Orlando Pirates
  5. Hat Trick Dhidi ya Coastal Yampa Mukwala Mzuka Kuelekea Dabi ya Kariakoo
  6. Matokeo ya Coastal Union vs Simba Leo 01/03/2025
  7. Kikosi cha Simba vs Coastal Union Leo 01/03/2025
  8. Coastal Union Vs Simba Leo 01/03/2025 Saa Ngapi?
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo