Mayele Aipeleka Pyramid Fainali Klabu Bingwa Afrika CAF

Mayele Aipeleka Pyramid Fainali Klabu Bingwa Afrika CAF

Mayele Aipeleka Pyramid Fainali Klabu Bingwa Afrika CAF

Fiston Mayele, aliyekuwa mshambuliaji maarufu wa Yanga, amejizolea umaarufu mpya baada ya kuipa timu yake ya Pyramids FC tiketi ya kucheza fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF) kwa kufunga mabao mawili muhimu dhidi ya Orlando Pirates. Mchezo ulichezeka Aprili 25, 2025, katika Uwanja wa Juni 30, jijini Cairo, Misri, na kumalizika kwa ushindi wa mabao 3-2 kwa Pyramids FC.

Mayele Aipeleka Pyramid Fainali Klabu Bingwa Afrika CAF

Katika mechi hio, Mayele aliibuka kua shujaa wa mchezo baada ya kufunga bao la ushindi dakika ya 84, akimalizia kwa shuti mpira uliotemwa na kipa Sipho Chaine wa Orlando. Pyramids ilikuwa ikilazimika kurudi nyuma mara mbili katika mchezo huu baada ya kutanguliwa kufungwa na Orlando Pirates. Licha ya changamoto hizo, Mayele alifanya kazi ya ziada kuhakikisha timu yake inapata ushindi.

Orlando Pirates walikuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 41 kupitia kwa Relebohile Mofokeng, lakini Pyramids hawakukata tamaa. Mayele alisawazisha bao hilo katika dakika za nyongeza za kipindi cha kwanza, na kuhakikisha hali ya mchezo inakuwa 1-1.

Kipindi cha pili kilianza kwa Orlando Pirates kupata bao la pili katika dakika ya 52 kupitia kwa Mohau Nkota, lakini Pyramids ilijibu kwa haraka, na Ramadan Sobhi alisawazisha katika dakika ya 57.

Katika hatua ya mwisho, ilimlazimu Mayele kutumia ufanisi wake wa kipekee kufunga bao la tatu katika dakika ya 84, ambapo alitumia nafasi aliyoipata baada ya kipa wa Orlando Pirates, Sipho Chaine, kutemwa mpira. Hii ilikuwa ni hatua ya mwisho ya mchezo na ilifanya Pyramids kufuzu kwa fainali kwa jumla ya mabao 3-2, huku mechi ya kwanza ikiwa imeishia sare tasa ya 0-0 nchini Afrika Kusini.

Kwa upande mwingine, mchezo mwingine wa nusu fainali ulivuta hisia nyingi ambapo Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini ilicheza dhidi ya Al Ahly katika Uwanja wa Kimataifa wa Cairo. Mamelodi Sundowns walivunja mfungo wa Al Ahly kwa kupitia kanuni ya bao la ugenini, baada ya mechi kumalizika kwa sare ya bao 1-1. Mamelodi walikuwa wameshinda kwa jumla kwa sababu ya sare ya 0-0 katika mechi ya kwanza. Bao la Al Ahly lilifungwa na Mohamed Taher, lakini Mamelodi walijibu kwa bao la kushtukiza dakika ya 89 kutoka kwa Yassr Ibrahim alijifunga, na hivyo kuwavusha Sundowns.

Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika 2024/2025 itakutanisha Pyramids FC dhidi ya Mamelodi Sundowns, ambapo mechi ya kwanza itachezwa nchini Afrika Kusini, Pretoria, mnamo Mei 24, 2025, na mechi ya marudiano itakuwa huko Cairo, Misri, tarehe Juni Mosi, 2025. Hii itakuwa ni fainali ya kipekee ambapo timu hizi zitachuana kwa ajili ya taji la Ligi ya Mabingwa Afrika.

Ushindi huu wa Pyramids FC ni wa kihistoria, na Mayele ameonyesha ubora wake katika mashindano haya ya kimataifa. Pyramids FC sasa inakabiliwa na changamoto kubwa ya kutwaa ubingwa, huku wakijiandaa kwa fainali ambayo itavutia mashabiki wa soka duniani kote.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Al Ahly Yamtimua Kocha Marcel Koller Baada ya Kutolewa Klabu Bingwa Afrika
  2. Mtibwa Sugar Yarejea Ligi Kuu NBC 2025/2026
  3. Timu Zilizofuzu Nusu Fainali Kombe la Muungano 2025
  4. JKU Yaiondoa Singida Black Stars Kombe la Muungano
  5. Wachezaji Saba Watimuliwa Zanzibar Kwa Tuhuma Za Kubeti
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo