Matokeo ya Zanzibar Heroes VS Kilimanjaro Stars leo 03/01/2024 | Matokeo ya Kilimanjaro Stars Dhidi ya Zanzibar Heroes leo Mapinduzi Cup 2025
PAZIA la michuano ya Kombe la Mapinduzi 2025 limefunguliwa rasmi leo kwa mchezo wa kusisimua kati ya Kilimanjaro Stars ya Tanzania Bara na Zanzibar Heroes, mechi iliyopigwa katika Uwanja wa Gombani, Pemba.
Michuano ya mwaka huu, ambayo imejumuisha timu za taifa badala ya klabu, imeanza kwa hekaheka nyingi kutokana na mabadiliko ya dakika za mwisho katika ratiba baada ya Uganda na Burundi kujiondoa.
Kutokana na kujitoa kwa timu za Uganda The Cranes na Burundi, waandaaji wa michuano walilazimika kupangua ratiba, na hivyo mchezo wa ufunguzi kuwa kati ya timu hizi mbili ndugu za Tanzania Bara na Zanzibar. Zanzibar Heroes wakiwa wenyeji wa michuano hii walikabiliana na changamoto ya kuandaa ratiba mpya kwa haraka ili kuhakikisha michuano inaendelea kama ilivyopangwa.
Matokeo ya Zanzibar Heroes VS Kilimanjaro Stars leo 03/01/2024
Zanzibar Heroes | VS | Kilimanjaro Stars |
- 🏆 #MAPINDUZI CUP
- ⚽️ Zanzibar Heroes🆚Kilimanjaro Stars
- 📆 03.01.2025
- 🏟 Uwanja wa Gombani
- 🕖 02:15 Usiku
Mchezo wa leo ulikuwa wa maana kwa pande zote mbili kuanza kwa kupata pointi muhimu. Timu mbili zitakazomaliza na pointi nyingi ndizo zitakazofuzu kucheza fainali itakayofanyika Januari 13, siku moja baada ya sherehe za miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Upinzani wa Jadi Kati ya Timu Hizi
Mchezo wa leo ulitabiriwa kuwa mgumu, na matarajio hayo yamejidhihirisha uwanjani. Timu zote mbili ziliundwa na wachezaji wanaotamba katika Ligi Kuu Tanzania Bara, ambayo kwa sasa imesimama kupisha michuano ya Kombe la Mapinduzi na Fainali za CHAN zinazotarajiwa kuanza mwezi ujao katika nchi za Kenya, Uganda, na Tanzania.
Vikosi vya Kilimanjaro Stars na Zanzibar Heroes vilikuwa na mazoezi ya mwisho jana chini ya makocha wao, Ahmad Ally kwa Kilimanjaro Stars na Hemed Suleiman ‘Morocco’ kwa Zanzibar Heroes. Wachezaji waliotarajiwa kung’ara kwa Kili Stars ni Crispin Ngushi, Edgar Williams, Ayoub Lyanga, Metacha Mnata, na Lusajo Mwaikenda. Kwa upande wa Zanzibar Heroes, nyota waliovutia macho ya wengi ni Feisal Salum ‘Fei Toto’, Laurian Makame, Maabad Maulid, na Ame Ibrahim.
Historia ya Upinzani wa Timu Hizi
Kumbukumbu zinaonyesha kuwa mara ya mwisho timu hizi zilipokutana, zilitoka sare katika mchezo wa ufunguzi wa Uwanja wa New Amaan Complex, Unguja. Hata hivyo, kila mchezo kati ya timu hizi huwa ni vita kutokana na upinzani wa kihistoria na umahiri wa wachezaji wao.
Ratiba ya Michuano
Michuano ya Kombe la Mapinduzi mwaka huu imepangwa kwa namna inayovutia, ikijumuisha timu nne pekee baada ya Burundi na Uganda kujiondoa. Mechi ya pili itakutanisha Burkina Faso dhidi ya Harambe Stars ya Kenya kesho usiku, huku Zanzibar Heroes wakitarajiwa kurejea uwanjani Januari 6 dhidi ya Burkina Faso. Kilimanjaro Stars wao watacheza na Kenya Januari 7, na mchezo wao wa mwisho wa hatua ya makundi utakuwa Januari 9 dhidi ya Burkina Faso.
Mapendekezo ya Mhariri:
Leave a Reply