Matokeo ya Yanga Vs Vitalo Leo 24/08/2024

Matokeo ya Yanga Vs Vitalo Leo 24/08/2024 Klabu Bingwa | Matokeo ya Yanga Leo Dhidi ya Vital’o CAF

Mabingwa watetezi wa Ligi kuu Tanzania bara, Klabu ya Yanga Sc leo itapambana na Vital’o ya Buruni katika mchezo wa marudiano wa michuano ya klabu Bingwa Afrika CAF katika uwanja wa Azam Complex Chamanzi leo Agosti 24 majira ya saa moja usiku.

Yanga, ambao walionyesha kiwango cha hali ya juu katika mechi ya kwanza ya michuano hii ya CAF Champions league 2024/2025 kwa kuwachapa Vital’o mabao 4-0, wanatazamiwa kuendeleza wimbi lao la ushindi mnene. Hata hivyo, kocha wao Miguel Gamondi ameonya kuwa bado hawajafuzu na wanapaswa kucheza kwa umakini mkubwa.

Mechi hii inatarajiwa kuwa yenye ushinani mkubwa kwani Vital’o watakuwa na kibarua kigumu cha kugeuza matokeo ya mechi ya kwanza. Kocha wao, Parris Sahabo, amesisitiza kuwa hawatakwenda kujilinda bali watacheza kwa kushambulia ili kutafuta mabao.

Kwa upande mwingine, Yanga wamepania kusaka ushindi mkubwa zaidi ili kujikusanyia mamilioni kutoka kwa ahadi ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kulipa shilingi milioni 5 kwa kila bao la ushindi katika mechi za kimataifa.

Matokeo ya Yanga Vs Vitalo Leo 24/08/2024

Yanga Sc 6-0 Vital’o

FT: YANGA SC 🇹🇿 6-0 🇧🇮 VITAL’O FC (Agg. 10-0)
⚽ Pacome 14′
⚽ Mzize 49′
⚽ Chama 51′
⚽ Dube 72′
⚽ Aziz Ki 78′

Yanga Sc itachuana na CBE SA ya Ethiopia kwenye raundi ya kwanza kutafuta tiketi ya hatua ya makundi ya CAFCL 2024/25.

  • 🏆 #Klabu Bingwa Afrika CAF
  • ⚽️ Young Africans SC VS Vital’O FC
  • 📆 24.08.2024
  • 🏟 Azam Complex
  • 🕖 Saa Moja Usiku

Angalia Hapa Kikosi cha Yanga Vs Vitalo Leo 24/08/2024

Matokeo ya Yanga Vs Vitalo Leo 24/08/2024

Kocha wa Yanga, Miguel Gamondi, ameweka wazi kuwa ingawa walishinda kwa kishindo katika mchezo wa awali, hawachukulii mchezo wa leo kwa wepesi. Akisisitiza umuhimu wa tahadhari, Gamondi amesema kuwa wapinzani wao Vital’O wanaweza kuleta changamoto mpya, hivyo Yanga inatarajia kutumia kikosi chao kamili ili kupata ushindi na kufuzu kwa hatua inayofuata.

Yanga imejipanga vilivyo kuhakikisha wanapata matokeo bora zaidi, huku ikilenga kuandika historia mpya ya michuano ya CAF. Katika mchezo wa kwanza, walionyesha kiwango cha juu cha soka, wakimiliki mpira na kuonyesha ubora wa kiufundi. Ushindi wa leo utaipa Yanga fursa ya kujiandaa kwa hatua zinazofuata katika michuano hii ya kimataifa.

Kwa upande wa Vital’O, ingawa walipoteza kwa mabao 4-0 katika mchezo wa awali, wamejipanga kwa mchezo wa leo kwa lengo la kulipiza kisasi. Kocha wa Vital’O, Parris Sahabo, amesema kuwa timu yake haitaingia uwanjani kwa nia ya kujihami pekee, bali watajaribu kutafuta bao la mapema ili kuleta presha kwa wenyeji wao, Yanga. Sahabo amesisitiza kuwa, licha ya ubora wa Yanga, vijana wake wanayo nafasi ya kufanya kitu cha tofauti na kuvutia macho ya mashabiki wa soka barani Afrika.

Waamuzi wa Mchezo

Mchezo huu utaamuliwa na waamuzi kutoka Gambia, wakiongozwa na Lamin Jamweh, ambaye atasaidiwa na Abdul Jawo na Nfally Jarju. Lamin, mwenye umri wa miaka 35, ana rekodi nzuri ya kuchezesha mechi za Ligi ya Mabingwa, huku akionyesha ustadi wa hali ya juu katika kutatua changamoto za kiufundi zinazoibuka uwanjani. Kwa mujibu wa takwimu, Lamin hajawahi kutoa kadi nyekundu mara kwa mara, jambo linaloonyesha kuwa ni mwamuzi anayependelea nidhamu na haki uwanjani.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Kikosi cha Yanga Vs Vitalo Leo 24/08/2024
  2. Vituo Vya Kununua Tiketi Mechi ya Yanga Vs Vitalo Klabu Bingwa
  3. Kikosi Cha Yanga VS Vitalo Leo 17/08/2024 CAF
  4. Matokeo ya Vitalo Vs Yanga Leo 17/08/2024 CAF
  5. Viingilio Mechi ya Vital O FC Vs Yanga Klabu Bingwa 17/08/2024
  6. Vituo vya Kukata Tiketi Mechi ya Ngao ya Jamii Yanga vs Simba
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo