Matokeo ya Yanga Vs Dodoma Jiji leo 25/12/2024

Kikosi cha Yanga Vs Dodoma Jiji leo

Matokeo ya Yanga Vs Dodoma Jiji leo 25/12/2024 | Matokeo ya Yanga leo dhidi ya Dodoma Jiji

Yanga leo itashuka dimbani saa 10:00 jioni kucheza dhidi ya wenyeji wao, Dodoma Jiji FC, kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma. Hii ni sehemu ya kampeni yake ya kutetea taji la ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, ambapo Yanga inalenga kulichukua kwa mara ya nne mfululizo. Kocha Mkuu wa Yanga, Sead Ramovic, amesema mchezo huu ni fursa ya kutoa zawadi ya Krismasi kwa mashabiki wao kupitia ushindi muhimu.

Kocha Ramovic amesisitiza kuwa lengo kuu la Yanga ni kupata pointi tatu muhimu. Ushindi wa leo utaiweka Yanga katika nafasi nzuri zaidi ya kuongoza msimamo wa Ligi Kuu, hasa baada ya kuwa na michezo mfululizo ya mafanikio. Yanga ina pointi 33 baada ya kushinda michezo 11 kati ya 13 iliyocheza msimu huu. Timu hiyo pia ina mabao 23 ya kufunga huku ikiruhusu mabao sita pekee, ikionyesha uimara wake katika safu ya ushambuliaji na ulinzi.

Hata hivyo, Ramovic alibainisha kuwa huenda akafanya mabadiliko madogo kwenye kikosi chake kutokana na uchovu wa wachezaji waliotumika kwenye michezo miwili iliyopita. Yanga ilishinda dhidi ya Mashujaa FC kwa mabao 3-2 na kuibuka na ushindi mkubwa wa 4-0 dhidi ya Prisons, michezo yote ikichezwa ndani ya muda mfupi kwenye Uwanja wa KMC Complex, Dar es Salaam.

Dodoma Jiji FC, inayoshika nafasi ya 15 kwenye msimamo wa Ligi Kuu kwa pointi 11 baada ya michezo 14, inakutana na changamoto kubwa ya kuwakabili mabingwa watetezi, Yanga. Kocha Mkuu wa Dodoma Jiji, Mecky Maxime, amewaonya wachezaji wake dhidi ya kufanya makosa ambayo yanaweza kuwapa Yanga nafasi ya kuadhibu.

“Tumekutana na timu nne kubwa kutoka Dar es Salaam msimu huu, mbili tumezifunga na mbili zimetufunga. Yanga ni timu ya tano, na itakuwa changamoto kubwa. Tunapaswa kuwa makini sana ili kuepuka makosa ambayo yanaweza kuigharimu timu,” alisema Maxime.

Licha ya changamoto zilizopo, Maxime ana matumaini kuwa wachezaji wake wataonyesha uimara wa kiufundi na kufuata maelekezo yake ili kufanikisha matokeo mazuri kwenye uwanja wa nyumbani.

Rekodi na Msimamo wa Timu Zote

  • Yanga SC: Pointi 33, ushindi mara 11, mabao 23 ya kufunga, mabao 6 kuruhusu.
  • Dodoma Jiji FC: Pointi 11, nafasi ya 15, ushindi mara moja tu tangu Novemba 3, 2024.

Matokeo ya Yanga Vs Dodoma Jiji leo 25/12/2024

Yanga Sc VS Dodoma Jiji
  • 🏆 #NBCPremierLeague
  • ⚽️ Dodoma Jiji🆚Young Africans SC
  • 📆 25.12.2024
  • 🏟 Jamhuri
  • 🕖 10:15 Jioni

Kikosi cha Yanga Vs Dodoma Jiji leo

Matarajio ya Mashabiki

Mashabiki wa Yanga wanatarajia timu yao kuendeleza rekodi nzuri kwa kupata ushindi wa leo. Kwa upande mwingine, mashabiki wa Dodoma Jiji wanategemea timu yao kutumia faida ya kucheza nyumbani ili kuvunja ukame wa ushindi wa muda mrefu.

Kwa ujumla, mchezo huu unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na umuhimu wa pointi tatu kwa pande zote mbili. Yanga inalenga kujiimarisha kileleni, huku Dodoma Jiji ikiwania kujiweka salama kwenye msimamo wa ligi.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Kikosi cha Yanga Vs Dodoma Jiji leo 25/12/2024
  2. Penati ya Dakika za Majeruhi Yaipa Simba Pointi Tatu Dhidi ya JKT
  3. Matokeo ya Simba vs JKT Tanzania Leo 24/12/2024
  4. Shaban Chilunda Awindwa na KMC
  5. Yanga Yaibuka na Pointi tatu Dhidi ya Tanzania Prisons
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo