Matokeo ya Yanga Princess vs Simba Queens Sc Leo 13/11/2024

Yanga Princess vs Simba Queens Sc Leo Saa ngapi

Matokeo ya Yanga Princess vs Simba Queens Sc Leo 13/11/2024 | Matokeo ya Yanga Princess Leo vs Simba Queens

BAADA ya mtanange maarufu wa ligi kuu ya NBC upande wa wanaume almaarufu kama Karikoo Dabi kumalizika Oktoba 19 mwaka huu katika dimba la Benjamin Mkapa, Dar ambapo mabingwa watetezi wa ligi kuu ya wanaume Yanga kushinda bao 1-0 dhidi ya Simba, hatimaye leo mashabiki wanatarajia kushuhudia mbabe kati ya waasimu hawa wawili kwa upande wa wanawake. Mechi hii inatarajiwa kuanza kutimua vumbi leo majira ya saa 10:00 jioni, huku pande zote zikijipanga kuonesha ubabe wao kwenye ligi kuu ya wanawake.

Mashabiki wa soka wamekuwa na shauku kubwa baada ya mtanange wa wanaume, na leo macho yote yanaelekezwa kwenye Karikoo Dabi ya wanawake ambapo Yanga Princess watachuana na Simba Queens katika uwanja huo huo maarufu wa Benjamin Mkapa.

Msimu huu, hizi timu zimekutana mara moja kwenye michuano ya Ngao ya Jamii, Oktoba 2, ambapo Yanga Princess waliibuka kidedea baada ya ushindi mnono wa mikwaju ya penalti 4-3 baada ya sare ya 1-1. Hivyo, pambano la leo linatarajiwa kuwa la kusisimua kwa sababu Simba Queens wameonyesha ubora wa hali ya juu tangu msimu uanze.

Kwa upande wa rekodi, Simba Queens wamekuwa na historia nzuri zaidi dhidi ya Yanga Princess katika Ligi Kuu ya Wanawake.

Kwa misimu mitano iliyopita, Yanga Princess haijafanikiwa kupata ushindi dhidi ya Simba kwenye ligi, huku ushindi wao wa mwisho ukiwa mwaka 2018 kwa bao 1-0 lililowekwa kimiani na Clara Luvanga. Tangu wakati huo, Yanga imekutana na Simba mara 12, na kutoka na ushindi mara moja tu, sare tatu, na kupoteza michezo mingine nane.

Kwa sasa, Simba Queens wapo kileleni mwa msimamo wa ligi kwa alama 9 baada ya kushinda michezo yote mitatu ya mwanzo.

Simba imekuwa ikiwafunga wapinzani wao kwa mabao mengi, ikiwemo ushindi wa 3-0 dhidi ya Mlandizi Queens, 3-1 dhidi ya Fountain Gate Princess, na 4-1 dhidi ya Ceasiaa Queens. Yanga Princess, kwa upande mwingine, wameanza kwa kusuasua kwenye msimu huu, wakipata sare tatu katika mechi zao za awali na kuwa na alama 3 pekee.

Matokeo ya Yanga Princess vs Simba Queens Sc Leo 13/11/2024

Yanga Princess 0-1 Simba Queens

Matokeo ya Yanga Princess vs Simba Queens Sc Leo 13/11/2024

Maandalizi ya Timu na Tathmini ya Makocha

Kocha wa Simba Queens, Yussif Basigi, amesema wanajiandaa kuingia uwanjani kwa malengo ya kupata pointi tatu muhimu ili waendelee kuimarisha nafasi yao kileleni. “Tunafahamu ni mchezo mgumu wa dabi, hivyo maandalizi tuliyofanya yanaendana na umuhimu wa mchezo huu. Tuna imani kuwa tutachukua pointi tatu,” alisema Basigi.

Aliongeza kuwa licha ya Simba kuwa na safu imara ya ushambuliaji, changamoto yao kubwa iko kwenye ulinzi kwani wamekuwa wakiruhusu mabao karibu kila mechi, na watafanya jitihada kuhakikisha wanakuwa thabiti zaidi leo.

Kwa upande wa Yanga Princess, kocha Edna Lema maarufu kama ‘Mourinho’ amesema mchezo wa leo ni nafasi ya kuonesha ubora wa timu yake licha ya changamoto walizopitia msimu huu.

“Simba ni timu yenye uwezo mkubwa, lakini nasi tunajiandaa kupata matokeo. Hatutazingatia sana matokeo ya nyuma, bali tunalenga kuongeza alama tatu na kujiweka nafasi nzuri kwenye msimamo wa ligi,” alisema Lema.

Mchezaji wa Kuzingatia – Jentrix Shikangwa

Jentrix Shikangwa, mshambuliaji hatari wa Simba Queens, amekuwa na mwendelezo mzuri wa kufunga mabao kwenye mechi za hivi karibuni. Yanga Princess wanahitaji kuwa na ulinzi thabiti kuweza kumzuia Shikangwa ambaye amejipambanua kuwa na uwezo wa kufumania nyavu. Kwa upande wa Simba, safu ya ushambuliaji inayojumuisha Shikangwa, Asha Mwalala, na Shelda Boniface inatarajiwa kuwa na mchango mkubwa katika mchezo wa leo.

Yanga Princess wamekuwa na changamoto katika kumalizia mashambulizi tangu msimu huu ulipoanza, na safu yao ya ushambuliaji inaonekana kukosa mshikamano. Washambuliaji kama Ariet Udong, ambaye anajulikana kwa kasi, nguvu, na uwezo wa kumiliki mpira, hajapata usaidizi wa kutosha kutoka kwa viungo, hali inayosababisha timu hiyo kukosa mabao. Kocha Lema atalazimika kutafuta njia ya kuboresha muunganiko wa timu ili waweze kuleta ushindani mkali dhidi ya Simba.

Mapendekezo ya mhariri:

  1. Yanga Princess vs Simba Queens Sc Leo 13/11/2024 Saa ngapi?
  2. Simba yatua bodi ya Ligi Kutaka Mabadiliko ya Ratiba
  3. Ratiba ya Taifa Stars Kufuzu AFCON 2025
  4. Kocha Moallin Amwaga Manyanga KMC
  5. Simba na Azam Ndio Wababe wa Kutoruhusu Magoli Ligi Kuu
  6. Tabora United Yavuna Milioni 20 Baada ya Kuichapa Yanga
  7. Kibwana Shomari Aomba Kuondoka Yanga
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo