Matokeo Ya Uhakiki Nactevet Waombaji Waliochaguliwa Awamu Ya Pili Septemba 2024/2025

Uhakiki NACTEVET

Matokeo Ya Uhakiki Nactevet Waombaji Waliochaguliwa Awamu Ya Pili Septemba 2024/2025 | Majibu ya Uhakiki NACTEVET (NACTE Student verification 2024/2025)

Matokeo Ya Uhakiki Nactevet Waombaji Waliochaguliwa Awamu Ya Pili

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET)limetangaza rasmi matokeo ya uhakiki kwa waombaji waliochaguliwa kujiunga na programu za ngazi ya Astashahada (Certificate) na Stashahada (Diploma) kwa muhula wa Septemba 2024. Matokeo hayo yanahusisha waombaji waliofanyiwa uhakiki wa awamu ya pili na yalitangazwa rasmi tarehe 7 Oktoba, 2024.

Jumla ya Waombaji Waliohakikiwa na Kuchaguliwa

Kwa mwaka wa masomo wa 2024/2025, NACTEVET imefanya uhakiki kwa jumla ya waombaji 45,540, ambapo kati yao wanawake ni 21,525 (47%) na wanaume ni 24,015 (53%). Mchakato huu ulifanyika kwenye vyuo mbalimbali vilivyokidhi vigezo vya kudahili wanafunzi.

Katika kundi hili, waombaji 44,088 (97%) walikidhi vigezo na kuchaguliwa kujiunga na programu mbalimbali, ambapo wanawake ni 20,722 na wanaume ni 23,366. Hata hivyo, waombaji 1,452 (03%) waligundulika hawakuwa na sifa zinazohitajika kwa programu walizoomba. Waombaji walio na sifa za kujiunga wanaweza sasa kuanza maandalizi ya safari yao ya masomo kwa kufuata taratibu zilizoainishwa.

Jinsi ya Kuangalia Majibu ya Uhakiki NACTEVET

Ili kuangalia matokeo ya uhakiki, waombaji wanaweza kufuata hatua zifuatazo:

1. Tembelea Tovuti Rasmi ya NACTEVET: Ingia kwenye tovuti ya Baraza kwa kubofya linki hii: NACTVET.

2. Chagua Uhakiki Muhula wa Septemba 2024: Baada ya kufungua tovuti, bofya kitufe kilichoandikwa “Uhakiki Muhula wa Septemba 2024”

Matokeo Ya Uhakiki Nactevet Waombaji Waliochaguliwa Awamu Ya Pili Septemba 2024/2025

3. Ingiza Msimbo wa Uhakiki: Andika msimbo wa uhakiki (code) uliotumwa kwenye namba ya simu uliotumia wakati wa maombi.

4. Thibitisha Wewe Sio Roboti: Kwenye sehemu ya kuthibitisha, ingiza msimbo unaoonekana kwenye picha kwa usahihi ili kuthibitisha kuwa wewe sio roboti, kisha bofya kitufe cha “Wasilisha”.

Uhakiki NACTE 2024

5. Angalia Matokeo Yako: Baada ya hapo, matokeo yako ya uhakiki yatatokea moja kwa moja.

Ni muhimu kwa waombaji kutunza msimbo waliotumiwa na Baraza kwani msimbo huo utatumika kwa ajili ya usajili wa chuo utakapoanza.

Maandalizi ya Usajili kwa Waombaji Waliochaguliwa

Baraza la NACTEVET limeagiza vyuo kuanza rasmi mchakato wa usajili wa wanafunzi waliopitishwa na Baraza kwa uhakiki. Usajili huu unatarajiwa kuanza rasmi tarehe 10 Oktoba na kumalizika tarehe 30 Novemba, 2024. Ili kufanikisha usajili, wanafunzi wanapaswa kufika vyuoni wakiwa na msimbo waliotumiwa kupitia namba zao za simu.

Vyuo vimeonywa kutofuata taratibu zilizowekwa za udahili kwani hatua stahiki zitachukuliwa dhidi ya chuo chochote kitakachokiuka miongozo iliyotolewa na Baraza. Hii ni kuhakikisha kuwa udahili unafanyika kwa kufuata sheria na kanuni zinazohusu elimu ya ufundi nchini.

Dirisha la Marekebisho kwa Waombaji Wasio na Sifa

Kwa waombaji ambao walifanyiwa uhakiki na kugundulika kuwa hawakukidhi vigezo katika programu walizoomba, Baraza limefungua dirisha maalum la marekebisho. Dirisha hili litakuwa wazi kuanzia tarehe 10 hadi 15 Oktoba, 2024. Waombaji waliokosa sifa katika programu walizoomba awali wanaweza kutumia fursa hii kuomba programu nyingine ambazo wanakidhi vigezo vyake.

Aidha, vyuo vinatakiwa kutumia kipindi hiki cha marekebisho kurekebisha taarifa za waombaji ambao taarifa zao hazikukamilika. Hii itasaidia kuhakikisha kuwa kila mwombaji anapata nafasi stahiki ya kujiunga na programu ambayo inaendana na sifa zake za kitaaluma.

Mwisho wa Mchakato na Msimbo Muhimu

Ni muhimu sana kwa waombaji waliopitishwa katika uhakiki kutunza msimbo wao wa uhakiki kwani utahitajika mara wanapofika chuoni kwa ajili ya usajili. Vilevile, Baraza limeagiza vyuo kuhakikisha kuwa wanafunzi wote wanaosajiliwa wamepitishwa na Baraza kupitia mchakato wa uhakiki.

Kwa taarifa zaidi, waombaji na vyuo vinaweza kuendelea kufuatilia tovuti rasmi ya NACTEVET au kufika ofisi za Baraza kwa maelekezo zaidi.

Bofya Hapa kupakua Tangazo la NACTEVET kuhusu Majibu ya uhakiki

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Ratiba ya Mtihani wa Kidato cha Pili 2024
  2. Majina ya Waliochaguliwa Kujiunga Vyuo vikuu Awamu ya Pili 2024/2025
  3. Majina ya Waliochaguliwa Chuo Cha UDSM Awamu ya Pili 2024/2025
  4. Majina ya Waliochaguliwa Chuo Kikuu Cha UDOM Awamu ya Pili 2024/2025
  5. Dirisha la Tatu la Maombi ya Vyuo Vikuu 2024/25: Tarehe 05 – 09 Oktoba
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo